ZARI Awashangaza Wengi Baada ya Tumbo lake la Uzazi Kupungua Ndani ya Wiki Moja...Atoa Ushauri Huu
USHAURI WA ZARI KWA WAZAZI from #zarithebosslady - Good morning.... ladies no need to worry coz our bodies are different. But I did exercise during pregnancy which has helped my body get bk within 7days.... and for those stretch marks keep using olive oil during and after pregnancy.
Bifu la Akikiba Na Dull sykes
BIFU la Alikiba na Dully Sykes...Alikiba Afunguka Haya
Mkali wa wimbo Aje Alikiba baada ya kuondoka na tuzo tatu za EATV, amefunguka na kuzungumzia mahusiano yake na msanii mkongwe wa muziki na producer, Dully Sykes. Hatua hiyo imekuja kutokana na kuenea kwa taarifa za muda mrefu katika mitandao ya kijamii kwamba wawili hao hawaelewani. Katika usiku wa tuzo za EATV, Dully ndiye aliyemtangaza mshindi wa video bora ya mwaka Alikiba kupitia video yake ya wimbo ‘Aje’ kabla ya kukabidhiwa tuzo na Katibu Mkuu wa Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) Godfrey Mngereza. Akiongea muda mfupi baada ya kuchukua tuzo hiyo akiwa pamoja na Dully Sykes, Alikiba alizishukuru tuzo hizo kwa kumkutanishwa na Dully Sykes huku akidai yeye anamchukulia kama baba katika muziki. “Mwenyezi Mungu leo ametukutanisha, huyu mimi ndiye aliyenianzisha, huyu ndiye aliyenifanya niamini mimi najua kuimba, nilichokuwa nikiimba brother Dully Sykes muda mwingine nilikuwa namtoa mpaka machozi,” Ali alikiambia kipindi cha Enewz cha EATV akiwa mbele ya Dully Sykes. “Nisipotokea siku mbili hata siku moja kwao lazima ataniulizia Ali yupo wapi. Sina simu sina nini, Dully Sykes alikuwa ananipenda sana sijajua sasa hivi lakini mimi kwangu Dully ni brother wangu na ninaweza nikamuita baba yangu wa kimuziki wa bongofleva. Mimi sina mengi ya kusema ila nataka ajue kwama mimi nampenda siku zote na nitampenda mpaka nakufa,” Naye Dully Sykes baada ya kusikia kauli hiyo ya Alikiba na yeye alisema hana tatizo na muimbaji huyo wa Aje na kusema anampenda pia.
DARASA AMKUNA PROFESA J
PROFESA Jay Akunwa Kisawa Sawa na Mwanamuziki Darasa Atoa ya Moyoni
Mafanikio ya Mwanamuziki Darasa kwenye muziki yamemfanya Prof Jay Kusema haya Kupitia mtandao wa Instagram, Jay ameandika: Mdogo wangu @darassacmg Imani yako, Kutokukata tamaa na Struggle yako ya Usiku na Mchana ndio imekufanya ufikie hapo ulipofikia, Nakumbuka wakati unashoot Wimbo wako wa USIKATE TAMAA uliniambia unatamani ufikie level za juu kama zetu, Nami nilikwambia hakuna kinachoshindikana chini ya JUA Ukiset GOALS, kufanya kazi kwa bidii na SALA yote Yanawezekana, Naamini kwa style hii ya JIWE juu Ya JIWE, NDOTO yako inakwenda kuwa kweli, Cha MSINGI usiridhike na mafanikio haya..HUU ni mwanzo tuu na mafanikio makubwa zaidi yako at your DOOR, Keep your eyes open and Keep ya HEAD UP, SKY IS THE LIMIT, GO GET DEM… BLESS #ACHA MANENO WEKA MUZIKI
Kamanda Sirro: Asema Aliyetishwa na kauli ya Mzee wa Upako afungue kesi
 Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam imemtaka yeyote anayeona kuwa kauli iliyotolewa na Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo maarufu Mzee wa Upako imetishia maisha yake, afungue kesi. Kamanda wa kanda hiyo, Simon Sirro aliyasema hayo jana Dar es Salaam wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari waliotaka kujua hatua polisi waliyoichukua kutokana na kauli aliyoitoa Mchungaji huyo kwamba waandishi waliomwandika vibaya watakufa kabla ya Machi mwakani. “Kama kuna mtu anaona katishika na kauli hiyo aje afungue kesi milango iko wazi. Kama kuna mwandishi yeyote anayeona ametishika na kauli hiyo aje, kesi ikifunguliwa tutaifanyia kazi kwa sababu hadi sasa hakuna aliyelalamika,” alisema. Kauli ya Mzee wa Upako aliitoa katika mahubiri yake ya Jumapili ikiwa ni mwendelezo wa majibu yake kutokana na tuhuma zilizoandikwa kwenye baadhi ya vyombo vya habari kwamba alimfanyia fujo jirani yake. Wakati huo huo, Sirro alisema kuwa wanaendelea na uchunguzi wa madai ya kupotea kwa Bernard Saanane ambaye ni kiongozi wa Chadema. Kiongozi huyo anadaiwa kupotea tangu Novemba 18. “Kuna watu wanasema wanataka ile miili ichunguzwe… lile ni tukio la Pwani na mwenye wasiwasi anaruhusiwa kuwasiliana na uongozi wa kule kwa sababu ule ni mkoa mwingine,” alisema. Hata hivyo, alipoulizwa kuhusu kukamatwa kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Forum, Maxence Melo alisema atazungumzia suala hilo Ijumaa.
Kanye West akutana na Donald Trump New York
Maamuzi ya Halmashauri kuu ya Taifa ya CCM
Haya Ndiyo Maamuzi Ya Halmashauri Kuu Ya Taifa Ya CCM Baada Ya Kikao Chake  Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM imekutana jana tarehe 13/12/2016 jijini Dar es salaam kwa kikao cha siku moja cha kawaida. Kikao hicho kimeongozwa na Mwenyekiti wa Taifa wa CCM Dkt. John Pombe Magufuli. Pamoja na mambo mengine, Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM imepokea taarifa ya Tathimini ya Uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, baada ya kuitafakari taarifa hiyo, Halmashauri Kuu imeamua yafuatayo;- 1. Kupunguza idadi ya wajumbe wa vikao na idadi ya vikao vya Chama katika ngazi mbalimbali ili kuongeza ufanisi wa utendaji wa Chama na kuongeza muda wa viongozi wa Chama kufanya kazi za Chama kwa Umma badala ya kutumia muda mwingi vikaoni. Ili kuwa na vikao vya Chama vyenye tija imeamuliwa kama ifuatavyo:- a). Halmashauri Kuu ya Taifa kwa sasa ina jumla ya wajumbe 388 idadi ambayo ni kubwa sana, hivyo imeamuliwa idadi hii ipunguzwe na kuwa wajumbe 158 kama ifuatavyo:- Wenyeviti wa Mikoa Mikoa ya Bara 26x1 = 26 Mikoa ya Zanzibar 6x1 = 6 Wajumbe wa NEC wa Mikoa Mikoa ya Bara 26x1 = 26 Mikoa ya Zanzibar 6x4 = 24 Wajumbe wa NEC wa Taifa Kutoka Bara = 15 Kutoka Zanzibar = 15 Nafasi za Mwenyekiti = 7 Wajumbe wa NEC wa Jumuiya UVCCM = 5 UWT = 5 WAZAZI = 5 Wajumbe wa NEC kutoka Bungeni = 5 Katibu wa Kamati ya Wabunge wa CCM = 1 Wajumbe wa NEC kutoka BLW = 3 Katibu wa Kamati ya Wawakilishi = 1 Wajumbe wa NEC – wanaotokana na Nyadhifa zao - Mwenyekiti wa CCM = 1 - Makamu Mwenyekiti (B) = 1 -Makamu Mwenyekiti (Z) = 1 - Makamu wa Rais = 1 - Waziri Mkuu = 1 - Makamu wa Pili wa Rais (Z) = 1 - Spika wa Bunge = 1 - Spika wa BLW = 1 - Mwenyekiti wa UWT = 1 - Mwenyekiti wa WAZAZI = 1 -Mwenyekiti wa UVCCM = 1 - Katibu Mkuu – WAZAZI = 1 - Katibu Mkuu – UWT = 1 - Katibu Mkuu – UVCCM = 1 Jumla: 158 #. Vikao vya kawaida vya Halmashauri Kuu ya Taifa vifanyike kila baada ya miezi sita badala ya miezi minne kama ilivyo sasa isipokuwa vinaweza kufanyika vikao maalum inapohitajika. b). Kwa upande wa sasa imeamuliwa wajumbe wa Kamati Kuu wawe 24 badala ya 34 kama ifuatavyo:- Mwenyekiti wa CCM. Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) Makamu wa Rais Katibu Mkuu wa CCM Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar) Waziri Mkuu Makamu wa Pili wa Rais (Z) Spika wa Bunge la Tanzania Spika wa BWL Mwenyekiti wa WAZAZI Mwenyekiti wa UWT Mwenyekiti wa UVCCM Katibu wa wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa Organaizesheni Katibu wa wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa Itikadi na Uenezi Katibu wa wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa Uchumi na Fedha Katibu wa wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Wajumbe watatu (3) wa kuchaguliwa na Halmashauri Kuu kutoka Tanzania Wajumbe watatu (3) wa kuchaguliwa na Halmashauri Kuu kutoka Zanzibar. #. Vikao vya kawaida vya Kamati Kuu vipunguzwe ili vifanyike kila baada ya miezi minne badala ya miezi miwili isipokuwa vinaweza kufanyika vikao maalum inapohitajika. c). Kwa ngazi ya mkoa, Wajumbe wa Kamati za Siasa za Mikoa wapunguzwe kwa kuondoa wajumbe watatu ambao ni:- Katibu wa Uchumi na Fedha wa Mkoa - 1 Wajumbe wa kuchaguliwa na H/Mkoa - 2 #. Vikao vya kawaida vya Kamati ya Siasa ya Mkoa vifanyike kila baada ya miezi mitatu badala ya kila mwezi kama ilivyo sasa isipokuwa vinaweza kufanyika vikao maalum inapohitajika. d). Kwa upande wa Wilaya Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Wilaya wapunguzwe kwa kuwoandoa:- Katibu wa Uchumi na Fedha wa Wilaya - 1 Katibu wa Kamati ya Madiwani - 1 Wajumbe wa kuchaguliwa na H/Kuu ya (W)- 2 Jumla: 4 #.Vikao vya kawaida vya Kamati ya Siasa ya Wilaya vifanyike kila baada ya miezi mitatu badala ya kila mwezi isipokuwa vinaweza kufanyika vikao maalum inapohitajika. #. Muundo wa Wilaya za Chama uendane na muundo wa sasa wa Serikali. Kata,Tawi na Shina Idadi ya kuanzisha Shina iwe wanachama 50 hadi 300. Idadi ya kuanzisha Tawi iwe wanachama kuanzia 301 hadi 1,000. Hata hivyo idadi hii izingatie eneo la kijiografia na wingi wa wanachama katika eneo hilo. Vikao vya kawaida vya Kamati za Siasa za ngazi hizi viwe vinafanyika mara moja kila baada ya miezi mitatu, isipokuwa vinaweza kufanyika vikao maalum inapohitajika. #. Nafasi za Uongozi Mwanachama anatakiwa kuwa na nafasi moja tu ya uongozi wa kazi za muda wote kama ilivyoainishwa kwenye Kanuni za uchaguzi wa Chama Toleo la 2012 kifungu cha 22 na 23 ambazo zimetajwa kuwa ni:- Mwenyekiti wa Tawi,Kijiji au Mitaa. Mwenyekiti wa Kata/Wadi. Mwenyekiti wa Jimbo, Wilaya na Mkoa. Makatibu wa Halmashauri Kuu wa ngazi zote zinazohusika. Mbunge, Mwakilishi na Diwani. #. Viongozi wa kuchaguliwa waepuke kuwa watendaji badala yake waongoze na kusimamia shughuli za Chama kwa kuzingatia Katiba na Kanuni. #.Vyeo ambavyo haviko kwenye Katiba Vyeo ambavyo havijatamkwa kwenye Katiba ya CCM haviruhusiwi katika Chama au Jumuiya zake mfano Umoja wa makundi mbalimbali kama Wenyeviti wa ngazi mbalimbali (mfano: Mwenyekiti wa Wenyeviti wa CCM n.k), Makamanda (UVCCM), Washauri (UWT) na Walezi (WAZAZI) katika ngazi zote. #. Uhakiki wa Wanachama wa CCM Halmashauri Kuu imeona ipo haja ya kufanya uhakiki wa wanachama wa CCM na Jumuiya zake ili kujua idadi sahihi ya wanachama wetu kwa wakati huu. Uhakiki huu uendane na kutoa kadi mpya za uanachama za kielektroniki ili kuwa na udhibiti wa usahihi wa wanachama na kuondoa wanachama HEWA. Aidha, Kadi za UWT, WAZAZI na UVCCM zifutwe ili tubaki na kadi za CCM tu. #. Jumuiya za Chama Cha Mapinduzi Jumuiya za CCM zimetakiwa kufanya kazi zake kwa kuzingatia matakwa ya Katiba ya CCM na Kanuni za Jumuiya husika, kanuni za Jumuiya ziendane na matakwa ya Katiba ya CCM. #.Uaendeshaji wa shughuli zote za Jumuiya za Chama na mali zake uwe chini ya usimamizi wa Chama Cha Mapinduzi. (Baraza la Wadhamini la Chama Cha Mapinduzi). Makatibu Wakuu wa Jumuiya watakuwa wanateuliwa na Kamati Kuu na Manaibu Katibu Wakuu watateuliwa na Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa. #. Wakati tukiendelea kubaki na Bendera yenye rangi ya kijani na njano na alama ya jembe na nyundo, Halmashauri Kuu imeona ipo haja ya kuzifanya rangi hizo kuwa na muenekano wa kuvutia zaidi. #. Utumishi katika Chama na Jumuiya zake. Katibu Mkuu wa CCM na Sekretarieti ipewe majukumu ya kusimamia ajira za Watumishi wa Chama na Jumuiya zake. Nafasi za Makatibu Wasaidizi wa Mikoa na Wilaya zitaondolewa na badala yake kazi zao zitatekelezwa na Makatibu wa Jumuiya za Chama wa Mikoa na Wilaya kwa utaratibu utakaopangwa. Utaratibu huu utakipunguzia Chama Cha Mapinduzi gharama na kujenga umoja wa utendaji kazi wa Chama na Jumuiya zake katika Mikoa na Wilaya. #. Tathimini ya hali ya Kisiasa na Uchaguzi wa Zanzibar . Halmashauri Kuu ya Taifa imeagiza kuundwa kwa Kamati maalum ya kufanya tathimini ya kina kuhusu hali ya kisiasa Zanzibar kwa ujumla na masuala yanayohusu uchaguzi wa Zanzibar 2015. # Mwenyekiti wa Kamati ya udhibiti na nidhamu ametakiwa akamilishe kazi ya taarifa ya udhibiti kwa wanachama waliokiuka mienendo ya kiuanachama kabla ya kuanza uchaguzi Mkuu wa Chama mwezi Februari 2017, Mikoa na Wilaya ambazo hazijaleta taarifa zao za kiudhibiti ziwe zimefikisha taarifa zao kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Udhibiti na Nidhamu kabla ya tarehe 30/01/2017. #. Uhakiki wa Mali za Chama uendelee kufanyika kwa kina na uchambuzi zaidi ukikamilika Taarifa yake iwasilishwe kwa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa mapema iwezekanavyo. #. Maamuzi na mapendekezo haya yatapelekea kufanyika kwa mabadiliko ya Katiba ya Chama na Kanuni za Jumuiya za Chama. #. Kwa mambo yale ambayo yatahitaji mabadiliko ya Katiba, Mkutano Mkuu utaandaliwa mapema mwakani na kutafakari na kupitisha mabadiliko hayo ya Katiba. Mwenyekiti wa CCM Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ameteua wafuatao kujaza nafasi mbalimbali ndani ya sekretarieti ambazo zimekuwa wazi kutokana na waliokuwa wakizishikilia kupewa majukumu mengine ya kiserikali. #.Ndg. Rodrick Mpogolo anakuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Ndg. Rajabu Luhwavi ambaye ameteuliwa kuwa balozi. #. Col. Ngemela Eslom Lubinga- Kuwa Katibu NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Dr. Asha-Rose Migiro aliyeteuliwa kuwa Balozi #. Humphrey Polepole kuwa Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Ndg. Nape Nnauye aliyeteuliwa kuwa Waziri. #. Wajumbe wengine watabaki kama walivyo sasa. Imetolewa na:- NAPE NNAUYE IDARA YA ITIKADI NA UENEZI 13/12/2016
YOUNG DEE ASEMA HATUMII MADAWA KUTUNISHA MUSULI SIRI YAKE NI MAZOEZI TUU
Magazet october21
                             
Ujenzi mpya Kagera Baada ya Tetemeko
Kagera yaanza kujengwa upya baada ya tetemeko  BAADHI ya majengo kama shule, hospitali na mengineyo yaliyoathiriwa na tetemeko la ardhi mkoani Kagera yameanza kujengwa na kufanyiwa ukarabati. Aidha, fedha zote za misaada zinazotolewa na watu mbalimbali wakiwemo wafadhili kutoka nchi za nje zinawekwa katika akaunti moja na kutumika baada ya kamati maalumu kupitisha matumizi yake kwa lengo la kuhakikisha zinatumika vizuri. Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Maafa katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Brigedia Jenerali Mbazi Msuya aliyasema hayo hivi karibuni alipozungumza na gazeti hili na kueleza kuwa uharibifu uliofanywa na tetemeko hilo ni mkubwa sana na misaada inayotolewa haiwezi kutosheleza mahitaji. Brigedia Jenerali Msuya alisema ukarabati wa majengo kama sekondari ya Ihungo na Nyakato pamoja na nyumba za walimu, umeanza pamoja na kujenga nyumba za muda za walimu hao wakati ukarabati ukiendelea. Alisema kinachofanyika ni fedha zote kuwekwa kwenye akaunti moja ya Maafa Kagera na kuna kamati maalumu inayozitoa na kuzigawa kulingana na mahitaji ya matumizi. Alisema kwa wafadhili waliojitokeza kujenga shule kama Ihungo na nyinginezo ambao ni wawili au watatu wanapeleka maombi katika Kamati ya Maafa mkoani humo ili kuruhusu fedha hizo nyingine kutumika katika sehemu nyingine iliyoathirika. “Uharibifu uliotokea ni mkubwa sana na serikali haina uwezo wa kumpatia kila mwananchi msaada, bali ni kufanya mambo yanayomgusa kila mmoja kama ujenzi wa shule, hospitali na zahanati na kuwapatia misaada mingine ya jumla,” alieleza Mkuu huyo wa Maafa nchini.
Je wajua madhara ya Mkojo mchafu (UTI)
Madhara ya tatizo la mkojo mchafu 11 hours ago  Mkojo mchafu (UTI) ni matatizo katika njia ya mkojo ambayo huchangiwa na maradhi na matatizo ya aina mbalimbali. Matatizo ya UTI husababishwa na vimelea (bacteria) ambavyo huingia katika njia ya mkojo. Ugonjwa huu huweza kumpata mtu yeyote pasipo kujali ni mwanaume au mwanamke. Hata hivyo mwanaume huweza kuhisi dalili za UTI mapema zaidi kuliko mwanaume hii ni kutokana na tofauti za kimaumbile. Wanawake kwa upande wao huathiriwa na UTI hasa kutokana na mfumo mzima wa maungo yao hususani katika mfumo wa njua ya mkojo kuwa na urahisi wa kuingiliwea na vimelea. Mathalani, mrija wa mkojo yaani urethra ya mwanamke ni fupi ukilinganisha na ya mwanaume na hivyo vijidudu au bacteria huweza kupata urahisi wa kuingia ndani. Chanzo cha UTI Tatizo hili husababishwa na vyanzo mbalimbali, lakini zaidi ni maambukizi yanayosababisha UTI ni 'e.coli' na vijidudu vingine vya magonjwa ya zinaa mfano (klamidia) na vijidudu vya kisonono. Virusi ambavyo husababisha tatizo hili ni kama vile 'herpes simplex' na 'cytomegalo virus' mbali na sababu hizo nyingine ni pamoja na kushiriki ngono na wanawake wanaume/ wanawake wengi kwa upande wa wanawake pia ni mojawapo ya chanzo cha tatizo hili kwa kiasi kikubwa. Wengine wanaopatwa zaidi na tatizo hili ni wale wenye tabia ya kufanya ngono au kuwaingilia wengine kinyume na maumbile. Dalili za UTI Dalili zake zinatofautiana kati ya mwanaume na mwanamke, mwanaume mwenye tatizo hili anaweza kukojoa mkojo wa njano sana kila wakati na unakuwa na harufu mbaya hata na wakati mwingine mkojo huambatana na damu. Mwanaume anaweza kutokwa na manii kwenye mkojo au anapojikamua haja kubwa, huhisi muwasho katika njia ya mkojo na ukiminya uume unahisi unauma na wakati mwingine unakuwa umevimba. Uume pia hulegea au unaposimama huuma, vile vile hupata maumivu unapotoa manii wakati wa tendo, lakini manii huweza kuambatana na damu. Athari kubwa kwa wanaume ni kupunguza nguvu za kiume na kuziba njia ya mkojo. Kwa wanawake wao hushambuliwa na maumivu ya tumbo chini ya kitovu, maumivu na na moto wakati wa haja ndogo, homa za mara kwa mara na kutetemeka. Wakati mwingine mwanamke huweza kuhisi kama ni malaria au taifodi, lakini pia myu mwenye UTI huisi kukojoa mara kwa mara pamoja na nyonga zote kuuma na kutokwa na uchafu ukeni unaoambatana na muwasho. Hata hivyo, ulaji wa tunda la tikiti maji kwa wingi huweza kusaidia kusafisha njia ya mkojo na kusaidia kuondokana na tatizo hilo. Ikiwa unasumbuliwa na tatizo hili unaweza kufika Mandai Herbalist Clinic iliyopo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam na utajipatia tiba bora na kutapata kupona tatizo hilo bila shaka.
Kupatwa kwa jua 1 sep 2016
KATIKA GAZETI TANDO HILI UTAWEZA KUJIPATIA HABARI MOTO MOTO KATIKA PICHA ZA MATUKIO MBALIMBALI KUTOKA NDANI NA NJE YA TANZANIA HASA YALE YANAYOGUSA MAISHA YA KILA SIKU YA MTANZANIA.LUGHA KUU INAYOTUMIKA HUMU NI KISWAHILI.
June 22, 2016
JUA KUPATWA KIPETE MWEZI SEPTEMBA MOSI 2016
Mtaalam wa Astronomia (Astronomy) kutoka Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) Dk. Noorali Jiwaji wa Kitivo cha Sayansi, Teknologia na Elimu ya Mazingira, akizungumza na wanahabari (Hawapo pichani) wakati wa kuelezea tukio hilo leo Juni 22.2016, Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu Mkuu wa chuo hicho kikuu Huria, Profesa Elifas Tozo Bisanda.
Mtaalam wa Astronomia (Astronomy) kutoka Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) Dk. Noorali Jiwaji wa Kitivo cha Sayansi, Teknologia na Elimu ya Mazingira, akizungumza na wanahabari (Hawapo pichani) wakati wa kuelezea tukio hilo leo Juni 22.2016, Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu Mkuu wa chuo hicho kikuu Huria, Profesa Elifas Tozo Bisanda.
Muonekano endapo mtumiaji atatumia kichujia jua maalum.
Ramani ya Afrika inavyoonekana pindi tukio hilo litalavyokuwa…
Ramani ya Tanzania inavyoonesha itakavyokuwa siku tya tukio.
*************
TUKIO kubwa la angani la kipekee la kupatwa kwa jua usawa wa Tanzania litatokea Septemba 1, 2016, kuanzia saa 4:17 asubuhi hadi Saa 7:56 adhuhuri.
Washabiki na wanataaluma wa anga kutoka duniani kote pamoja na wanasansi, wanafunzi pamoja na jamii ya watanzania wataelekea Rujewa, kusini mwa Tanzania, Karibu na Mkoa wa Mbeya kushuhudia duara la jua linavyobadilika kuwa pete ya jua. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
Nchini kote Tanzania mamilioni ya watu watashangaa kuona jua kali la utosi likimegwa kwa zaidi ya asilimia 90 kwa kufunikwa na mwezi katika kupatwa kwa jua lionekane kama hilali nyembamba au kama mwezi mwandamo.
Katika tukio hili la kupatwa kwa jua, watu wanaoishi ndani ya ukanda wenye upana wa kilomita 100 unaokatisha Kusini ya Tanzania kutoka Congo kuelekea Katavi, mbeya, Ruvuma hadi Masasi na kuingia Msumbuji, siku hiyo jua kama duara jembamba kama pete kwa vile asilimia 98 ya jua litakuwa limejificha nyuma ya mwezi.
Kupatwa huko kwa jua kunaweza kuonekana kwa usalama na watazamaji, lakini inabidi kutumia vichuja maalum vya mwanga wa jua.
Tukio la kupatwa ni la kusisimua na la nadra sana kutokea katika maisha ya mtu. Hasa kwa kizazi hiki kipya ambacho kimechangamka kitasisimuliwa sana na tukio la ajabu kama hili na watajifunza Sayansi ili kuelewa kwa nini kinatokea kile wanachokiona.
Kwa hiyo tukio hili linaweza kutumiwa na shule na taasisi za elimu kuendeleza Sayansi na kuvuta wanafunzi kujiendeleza kisayansi na hasa kuelewa mizunguko mbalimbali iliyopo katika mfumo wetu wa sayansi pamoja na anga za juu kwa ujumla. Kuongeza uelewa wa sayansi ni muhimu katika kuelewa maumbile ya ulimwengu wetu.
Kupatwa huku kutatokea siku ya alhamisi ambapo wanafunzi wengi watakuwa mashuleni na ni wakati wa masomo.
Kwavile mchakato wote utaendelea kwa saa nne hivi , kati ya Saa 4 asubuhi hadi Saa 8 mchana wanafunzi wataweza kushirikiana kuangalia na kusimulia na kujadili tukio ili kulielewa vizuri na kuandika ripoti madarasani kwao.
Tukio jingine kubwa la kupatwa kwa jua kama hili halitatokea jingine kwa miaka 15 ijayo, kwa hiyo tunahitaji kutumia fursa hili kwa ukamilifu.
Ili kluangalia kupatwa huko, kila mmoja atahitaji kutumia kikinga macho kinachochuja mwanga wa jua kiitwacho kitazamia jua. Nihatari sana kuangalia jua kwa macho ya moja kwa moja au hata kutumia vichujio vingine vya kiza vilivyotengenezwa kibinafsi.
Kitazamia jua maalum ni kifaa rahisi kilichotengenezwa kutokana na kichuja nguvu ya jua ambacho kinaondoa mionzi haribifu kwa asilimia 99.999. Miwani hiyo maalum ya jua inaweza kutengenezwa Tanzania kwa gharama isiyozidi 500/= kila moja, ikiwemo kuchapa fremu za kadbodi na kichuja nguvu ya jua (polymer filter) kinachoagizwa kutoka Marekani.
Aidha wataalam wanaonya wananchi kutumia tahadhari kwa kutoanaglia tukio hilo moja kwa moja kwa macho yao kwani ni hatari na wanapaswa kutumia miwani maalum ya jua iliyotengenezwa maksusi kwa kazi hizo
Magazeti
ULIMISS HII YA JOH MAKINI KAZITAJA COLLABO ZAKE ZA INTERNATIONAL ITAZAME HII VIDEO HAPA CHINI…
Sababu zinazifanya samaki kupungua ziwaTanganyika
Sababu ya samaki kupungua Ziwa Tanganyika
ImageGETTY IMAGESImageWatu waliongezeka eneo hilo miaka ya 1990 kutokana na ongezeko la wakimbizi
Utafiti mpya umebaini kupungua pakubwa kwa idadi ya samaki katika Ziwa Tanganyika, mojawapo ya maziwa muhimu zaidi kwa uvuvi duniani, kumetokana na ongezeko la joto duniani katika karne moja iliyopita.
Ziwa Tanganyika ndilo la kale zaidi Afrika na samaki wake huwa muhimu sana kwa lishe katika mataifa yanayopakana na ziwa hilo.
Lakini idadi ya samaki imepungua sana, huku wavuvi wakiendelea kuongezeka.
Ongezeko hili la wavuvi lilidhaniwa kuwa chanzo kikubwa cha kupungua kwa idadi ya samaki.
Lakini utafiti mpya unaonesha chanzo hasa ni ongezeko la joto duniani kutokana na mabadiliko ya tabia nchi.
Ziwa Tanyanyika ndilo la pili kwa ukubwa duniani miongoni mwa maziwa yenye maji yasiyo na chumvi na maji yake huwa katika mataifa manne: Burundi, Jamhuri ya KIdemokrasia ya Congo, Tanzania na Zambia.
Samaki kutoka kwa ziwa hilo hutoa asilimia 60 ya protini zitokanazo na wanyama ambazo huliwa na watu eneo hilo.
Aidha, ni eneo lenye aina nyingi ya wanyama na mimea.
ImageGETTY IMAGESImageSamaki kutoka Ziwa Tanganyika hutegemewa sana na wakazi
Ili kufahamu mabadiliko yanayotokea katika ziwa hilo, watafiti wamechukua sampuli za mchanga kutoka kwenye kina cha ziwa hilo.
Baada ya kufanya utathmini wa mchanga huo na visukuku, wamepata viashiria kwamba idadi ya samaki imekuwa ikishuka sambamba na ongezeko la joto duniani.
Wanasayansi wanasema katika maziwa yanayopatikana maeneo yenye joto karibu na ikweta, ongezeko la joto katika maji hupunguza kuchanganyikana kwa maji kutoka sehemu ya juu ya ziwa ambayo huwa na oksijeni pamoja na maji yenye virutubisho vingi sehemu ya chini kwenye ziwa.
Kutochanganyikana vyema kwa maji haya husababisha virutubisho vinavyofika juu kwenye ziwa kupungua, hili hupunguza ukuaji wa miani (mimea ya rangi ya kijani, kahawia au nyekundu inayoota chini ya bahari) na hili hupelekea kupungua kwa lishe ya samaki.
Watafiti waliohusika katika utafiti huo wanasema ongezeko la joto limepunguza kuchanganyikana kwa maji, kupungua kwa ukuaji wa miani pamoja na kupungua kwa maeneo ambayo viumbe waishio chini ya bahari wanaweza kuishi na kustawi.
"Wazo letu lilikuwa kuchunguza visukuku na kubaini kushuka kwa idadi ya samaki kulianza wakati gani," anasema Prof Andrew Cohen kutoka Chuo Kikuu cha Arizona.
"Iwapo hili lilifanyika kabla ya kuanza kwa uvuvi wa kiviwanda miaka ya 1950, basi ungekuwa na ushahidi mkubwa kwamba hili halitokani na ongezeko la uvuvi na hivi ndivyo tulivyobaini."
Wanasayansi hao hata hivyo hawajapuuzilia mbali athari za ongezeko la uvuvi katika miongo sita iliyopita.
Wanasema kumekuwa an ongezeko la watu tangu miaka ya 1990, hasa kutokana na wakimbizi waliotoroka mizozo na kuhamia maeneo yaliyo karibu na ziwa hilo.
ImageGETTY IMAGESImageWavuvi hutumia taa kuwavutia dagaa, ambao ndio sana huvuliwa kutoka kwenye ziwa hilo
"Ukizingatia mtindo wa sasa wa kuendelea kugawika zaidi kwa maji kwenye ziwa, idadi ya samaki itaendelea kupungua. Watu wanaosimamia sera wanafaa kuanza kufikiria kuhusu chanzo mbadala cha mapato na lishe kwa watu wanaoishi eneo hilo."
Matokeo ya utafiti huo yamechapishwa katika jarida la kisayansi la Proceedings of the National Academy of Sciences.