ZARI Awashangaza Wengi Baada ya Tumbo lake la Uzazi Kupungua Ndani ya Wiki Moja...Atoa Ushauri Huu
USHAURI WA ZARI KWA WAZAZI from #zarithebosslady - Good morning.... ladies no need to worry coz our bodies are different. But I did exercise during pregnancy which has helped my body get bk within 7days.... and for those stretch marks keep using olive oil during and after pregnancy.
Bifu la Akikiba Na Dull sykes
BIFU la Alikiba na Dully Sykes...Alikiba Afunguka Haya
Mkali wa wimbo Aje Alikiba baada ya kuondoka na tuzo tatu za EATV, amefunguka na kuzungumzia mahusiano yake na msanii mkongwe wa muziki na producer, Dully Sykes. Hatua hiyo imekuja kutokana na kuenea kwa taarifa za muda mrefu katika mitandao ya kijamii kwamba wawili hao hawaelewani. Katika usiku wa tuzo za EATV, Dully ndiye aliyemtangaza mshindi wa video bora ya mwaka Alikiba kupitia video yake ya wimbo ‘Aje’ kabla ya kukabidhiwa tuzo na Katibu Mkuu wa Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) Godfrey Mngereza. Akiongea muda mfupi baada ya kuchukua tuzo hiyo akiwa pamoja na Dully Sykes, Alikiba alizishukuru tuzo hizo kwa kumkutanishwa na Dully Sykes huku akidai yeye anamchukulia kama baba katika muziki. “Mwenyezi Mungu leo ametukutanisha, huyu mimi ndiye aliyenianzisha, huyu ndiye aliyenifanya niamini mimi najua kuimba, nilichokuwa nikiimba brother Dully Sykes muda mwingine nilikuwa namtoa mpaka machozi,” Ali alikiambia kipindi cha Enewz cha EATV akiwa mbele ya Dully Sykes. “Nisipotokea siku mbili hata siku moja kwao lazima ataniulizia Ali yupo wapi. Sina simu sina nini, Dully Sykes alikuwa ananipenda sana sijajua sasa hivi lakini mimi kwangu Dully ni brother wangu na ninaweza nikamuita baba yangu wa kimuziki wa bongofleva. Mimi sina mengi ya kusema ila nataka ajue kwama mimi nampenda siku zote na nitampenda mpaka nakufa,” Naye Dully Sykes baada ya kusikia kauli hiyo ya Alikiba na yeye alisema hana tatizo na muimbaji huyo wa Aje na kusema anampenda pia.
DARASA AMKUNA PROFESA J
PROFESA Jay Akunwa Kisawa Sawa na Mwanamuziki Darasa Atoa ya Moyoni
Mafanikio ya Mwanamuziki Darasa kwenye muziki yamemfanya Prof Jay Kusema haya Kupitia mtandao wa Instagram, Jay ameandika: Mdogo wangu @darassacmg Imani yako, Kutokukata tamaa na Struggle yako ya Usiku na Mchana ndio imekufanya ufikie hapo ulipofikia, Nakumbuka wakati unashoot Wimbo wako wa USIKATE TAMAA uliniambia unatamani ufikie level za juu kama zetu, Nami nilikwambia hakuna kinachoshindikana chini ya JUA Ukiset GOALS, kufanya kazi kwa bidii na SALA yote Yanawezekana, Naamini kwa style hii ya JIWE juu Ya JIWE, NDOTO yako inakwenda kuwa kweli, Cha MSINGI usiridhike na mafanikio haya..HUU ni mwanzo tuu na mafanikio makubwa zaidi yako at your DOOR, Keep your eyes open and Keep ya HEAD UP, SKY IS THE LIMIT, GO GET DEM… BLESS #ACHA MANENO WEKA MUZIKI
Kamanda Sirro: Asema Aliyetishwa na kauli ya Mzee wa Upako afungue kesi
 Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam imemtaka yeyote anayeona kuwa kauli iliyotolewa na Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo maarufu Mzee wa Upako imetishia maisha yake, afungue kesi. Kamanda wa kanda hiyo, Simon Sirro aliyasema hayo jana Dar es Salaam wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari waliotaka kujua hatua polisi waliyoichukua kutokana na kauli aliyoitoa Mchungaji huyo kwamba waandishi waliomwandika vibaya watakufa kabla ya Machi mwakani. “Kama kuna mtu anaona katishika na kauli hiyo aje afungue kesi milango iko wazi. Kama kuna mwandishi yeyote anayeona ametishika na kauli hiyo aje, kesi ikifunguliwa tutaifanyia kazi kwa sababu hadi sasa hakuna aliyelalamika,” alisema. Kauli ya Mzee wa Upako aliitoa katika mahubiri yake ya Jumapili ikiwa ni mwendelezo wa majibu yake kutokana na tuhuma zilizoandikwa kwenye baadhi ya vyombo vya habari kwamba alimfanyia fujo jirani yake. Wakati huo huo, Sirro alisema kuwa wanaendelea na uchunguzi wa madai ya kupotea kwa Bernard Saanane ambaye ni kiongozi wa Chadema. Kiongozi huyo anadaiwa kupotea tangu Novemba 18. “Kuna watu wanasema wanataka ile miili ichunguzwe… lile ni tukio la Pwani na mwenye wasiwasi anaruhusiwa kuwasiliana na uongozi wa kule kwa sababu ule ni mkoa mwingine,” alisema. Hata hivyo, alipoulizwa kuhusu kukamatwa kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Forum, Maxence Melo alisema atazungumzia suala hilo Ijumaa.