Episode 1 & 2
RIWAYA: I HATE YOU MR. PRESIDENT ( 01 & 02 )
NA HUSSEIN O. MOLITO
O718 97 56 59, 0765 68 48 70
Mtawanyiko wa mawingu mekundu ndio ulioibadilishwa taswira ya mchana na kuwa usiku baada ya dakaki kadhaa kupita. Taa mbali mbali ziliwashwa kuashiria kua msaada wa jua haukuwepo tena na mwanga wa mwezi ulipo juu hautoshi kulifanya anga kuwa na nuru ya kutosha.
Sauti ya mwanamke aliaye kua akilia kwa uchungu ilisikika kwenye chumba chake huku hakuna mtu mwengine aliyekua anazijali zaidi ya mtoto wake pakee aliyekua pembeni yake akilia huku akihangaika bila kujua ni kitu gani kilichompata mama yake.
“tumbooo…. Naumiaaaaa… Mungu nisaidiee…nisaidie mimiiiiii”
Aliendelea kulia mwanamke huyo ambaye huku aki hangaika na tumbo lake kubwa lililoonekana kuwa na ujauzito usiopungua miezi Tisa.
“Baba…. Baba….”
Aliita Yule mtoto baada ya kwenda kugonga kwenye chumba cha pili kwa muda mrefu bila mafanikio. Alifanya hivyo mara kadhaa kila aliporudi na kumkuta mama yake akiwa kwenye hali mbaya kama hiyo.
Kilio hicho kilichoambatana na uchungu mkubwa au patao mwanamke huyo, ndio uliomfanya ajaribu kutambaa angalau atoke nje.
“mama…. Tuliaa.. utapona.”
Aliendelea kuongea Yule mtoto mdogo huku akilia na yeye kwa uchungu kwa jinsi alivyokua anamuona mama yake anavyoteseka kwa maumivu ayapatayo.
Chumba cha tatu alikaa mtoto mdogo wa mwenye nyumba hiyo. Aliamka na baada ya kusikia sauti za watu hao waliokua wakilia huku yule mtoto akim bembeleza mama yake.
Aliamka Yule mtoto wa chumba kingine na kwenda kwenye chumba hicho na kumsaidia kupiga simu kwenye hospital moja ya karibu na muda mfupi baadae gari ya kubebea wagonjwa ilifika kwenye nyumba hiyo.
Kwa kushirikiana na mlinzi wa getini. Waliweza kumbeba mgonjwa huyo na kumpandisha kwenye kitanda maalumu na kumpandisha kwenye gari hiyo tayari kwa kumuwahisha hospitalini.
Alipofika huko alipokelewa haraka na kuwahishwa kwenye chumba maalumu kilichopo kwenye ward ya wazazi.
“Eliyasa…. Tulia. Usiwe na wasi. Mama yako atapona tu.” Aliongea Yule mtoto wa kike aliyewasaidia baada ya Yule mtoto ELIYASA kuambiwa asubiri nje kwa muda usiojulikana.
Eliyasaa alijiinamia huku akiwa na mawazo mengi sana kuhusuiana na hali aliyokua nayo mama yake. Japokua alikua ni mtoto mdogo mwenye umri wa miaka saba tu, lakini alielewa kila kitu kutokana na maisha aliyoyapitia toka siku aliyoletwa duniani.
Simu ya Yule mtoto wa kike iliita na alipoangalia kwenye kioo cha simu yake. Jina la Lovely daddy lilitokea na kumfanya mtoto huyo asimame.
“baba ananihitaji, nitarudi tena kesho.”
Aliongea huyo msichana bila kuipokea simu ya baba yake na kuondoka zake na kumuacha Eliyasa akiwa amejiinamia huku akilia kiume. Hakutoa sauti ila machozi pekee yalidhihirisha maumivu aliyokua nayo juu ya maisha ya mama yake.
*****************************
Baada ya Yule mtoto kufika nyumbani kwao. Alimkuta baba yake akiwa kwenye mlango wa kuingilia sebuleni usiku huo huku akiwa amekunja sura . hakuwahi kukasirika mbele yake kama alivvyokasirika siku hiyo.
“hivi YASINTA, niongee na nini ili uelewe kua unahitajika kuwa mbali na ile familia?.... sasa kilichokupeleka huko ni nini?” aliongea baba yake kwa ukali.
“hicho ndicho kilichokufanya ukasirike baba. Wale ni viumbe na Mungu katuumba na roho za kuhurumiana sisi kwa sisi. Bila kujali kua wao hawana thamnani kama yetu hapa duniani.lakini kwa Mungu tuna thamani sawa baba.” Aliongea Yule mtoto mdogo mwenye umri wa miaka Tisa.
“hivi unataka tuwahurumie kwa kiwango gani. Hivi unafikiri nikiwa fukuza nyumbani kwangu watapata wapi hifadhi wale. Halafu jitu linafanya umalaya wakati anasaidiwa tu hapa. Wewe ungemuacha ajifungue hapa kwa shida ndio siku nyingine angeacha umalaya wake na kuzuia mimba nyingine. Sasa nakupa onya la mwisho… sihitaji kukuona ukiwa kariribu na familia ile. Sihitaji …sihitaji. Nimerudia mara zote hilo ili kukuonyesha ni jinsi gani nilivyokataa swala la wewe kushirikiana nao. Na kama utakiuka na kuwa nao. Utawaponza.”
Aliongea baba yake na kurudi chumbani kwake kwa hasira.
“kwanini baba anakua na roho ya kikatii kiasi hiki kwa viumbe hawa wa Mungu. Hata kama wamekosa. Angewasamehe tu.”
Aliongea peke yake huku kichwa chake kikiwa bado hakijaafikiana na baba yake juu ya kuwaacha watu hao wanaishi nyumba moja lakini maisha yao yakiwa yana utofaut mkubwa.
****************************
Juhudi za madaktari katika kuokoa maisha ya mama yake Eliyasa zilizidi kugonga mwamba baada ya kugundua kua anapoteza kiwango kikubwa cha damu.
“hata Benk yetu ya damu nayo imeishiwa… tufanyeje Dokta.” Aliongea mmoja wa manesi aliyekua anamuwekea damu mama yake Elyasa.
“hatuna budi… muite ndugu yake na tuongee nae atafute damu kwa ajili ya maisha ya mtu wao. Wakati sisi tunaendelea na utafiti wa mimba yake ikiwemo kumuwekea maji ya uchungu ili ajifungue haraka.” Alishauri dokta na nesi akatoka haraka na kumkuta Yule dogo akiwa amejiinamia.
“mtoto…kuna ndugu yenu mwengine mkubwa zaidi yako ambaye tunaweza kumpata kwa muda huu?” aliuliza Nesi baada yakumshtua Eliyasa.
“mimi ndio ndugu yake pekee ambaye naweza sema kua natakiwa kujua chochote kuhusu mgonjwa wangu.” Aliongea mtoto huyo kijasiri na kumfanya mpaka nesi kumshangaa kwa jinsi alivyonyoosha maelezo.
“nifuate.”
Aliongea nesi maneno hayo na Eliyasa bila kusubiri alianza kumfuata na kuingia nae kwenye chumba alicholazwa mama yake na kumuona akiwa macho lakini akiwa na dripu mbili za damu zikiingia mwilini kwake kwa pamoja.
“mama yako anahitaji damu nyingi sana ili tuokoe maisha yake. Na sisi uwezo wetu ni chupa nne za damu. Tumepungukiwa na chupa tatu. Sasa unatakiwa hivi sasa tukupime ili tujue kama unaweza kumtolea damu mama yako japo chupa moja. Na baadae upate msaada kwa wasamaria wema ili tuweze kumsaidia.”
Aliongea Daktari baada ya kuhakikisha kua hakuna mtu mwengine anayeweza kufanya hivyo zaidi ya mtoto huyo aliyejitambulisha kuwa huyo mgonjwa ni mama yake.
“nipo tayari mtoe hata hizo chupa tatu kama zitawezekana.. ninachokihitaji ni uhai wa mama yangu na mdogo wangu aliyekuwepo Tumboni.”
Aliongea mtoto huyo kwa sauti iliyojaa uchungu huku akimuangalia mama yake ambaye hakuweza kuongea kitu zaidi ya kutoa machozi tu huku akiona ni jinsi gani mtoto wake alivyojibebesha msalaba mzito kuliko umri wake.
Daktari alimchukua na kwenda kumpima japo kua alikua anajua kua umri wa mtoto huyo haujafikia hatua ya kutoa damu. Ila kwakua hakuna aliyekua na damu group O kwa wakati huo, waliamini kua huyo mtoto anaweza kuwa na damu itakayoweza kusaidia kuokoa maisha ya mama yake.
“oooh shiiiit”
Ulikua mguno wa daktari baada ya kugundua kua damu ya mtoto huyo ilikua haiendani na damu ya mama yake.
“inatakiwa uandike bango au kwenda kuomba watu wenye damu group O huko unapokwenda. Maana bila kufanya hivyo maisha ya mama yako yapo hatarini.”
Alishauri Daktari baada ya kumpa ukweli Yule mtoto. Bila kuaga, aliingia uswahilini na kuokota boksi kubwa aliloliandika kwa maandishi makubwa kwa maker pen.
“kila mwenye uchungu na mama yake. Basi anisaidie damu ya kumuokoa mama yangu. Kama una damu group O, basi ndio muokozi wa maisha ya mama yangu na mlezi wangu pekee.”
Bango hilo alilikamata na kupita nalo mitaani. Lilikua na ujumbe mzito sana uliogusa watu wengi waliojitokeza na kumuuliza kwa nini aliamua kuandika vile.
Nusu saa baadae, madaktari walishangaa kuona kundi la watu wapatao hamsini wakiongozana na Yule mtoto wakiwa tayari kutoa damu.
Tabasamu la daktari lilimpa mtuamaini mtoto huyo kua kuna uwezekano maisha ya mama yake na mdogo wake aliyekua tumboni yanaweza yakaendelea na kifo kika kaa mbali nao.
Idadi hiyo ya watu iliisaidia hata benki ya hospitali hiyo iliyofilisika damu ya group O kuongezeka kwa kasi kutokana na motto huyo.
Kila dakika isogeayo, ndio hatua za uwezekano wa kumrudisha mama yake katika haliya kawaida inavyozidi kuendelea vizuri.hatimaye yale maji ya uchungu waliyomuwekea yalifanya kazi na kusababisha aanze kulalamika na baadae kujifungua kwa njia ya kawaida.
“hongera. Umefanikiwa kokoa maisha ya mama yako na mdogo wako wa kiume.”
Aliongea Daktari na kumsababishia mtoto huyo kulia machozi ya furaha.
“kweli dokta?” aliuliza tena ili apate uhakika wa kile alichokisikia.
“kweli.. wewe ni mtoto jasiri sana. Nakutabiria makubwa sana kwenye maisha yako.” Aliongea Daktari na kuonyesha wazi kua alikua amefurahia uwepo wa mtoto huyo maeneo hayo.
“naweza kumuona?” aliuliza baada ya kuwa na hamu ya kumuona mama yake.
“unaweza kumuona. Yupo vizuri kabisa.”
Aliruhusu daktari na mtoto huyo alibisha hodi kwenye chumba cha mama yake.
“karibu muokozi wangu”
Aliitikia mama yake baada ya kuisikia sauti ya Eliyasa. Alikua anaijua kama tebo ya pili. Kila mara alipenda kuwa karibu na mwanaye huyo.
Alifika mtoto huyo huku michirizi ya machozi ikiwa katika mashavu yake. Hakuamini kua ni kweli aliyeitoa sauti yake kumkaribisha ni mama yake. Roho ilimuuma sana baada ya kuona dripu ya damu ikiendelea kuingia katika mwili wa mama yake.
“wewe ni shujaa wa dunia yangu, sijui vitu nilivyotendewa na wazazi wangu toka na zaliwa. Ila hiki ulichokitenda mwanangu ni zaidi ya mtu yeyote aliyewahi kutenda kitu kizito kama hiki atika maisha yangu. Nakupenda sana mwanangu. Daima nayasahau machungu ya baba yako kila nikuonapo. Haujawahi kunikosea. Ila hata mimi sijakosea kukuzaa wewe. Ila aliyenipa mimba ndio mwenye makosa ya kukufanya uishi kwa tabu bila sababu kiumbe wa Mungu.”
Alilalamika mama huku machozi yanamtoka na kumfanya mtoto huyo kuzidi kulia kwa kwikwi.
“usiyamalize machozi yako mwanangu wakati nipo hai. Siku nikifa utalia nini?... acha machungu ya dunia yapite, nina imani faraja ipo mbele yetu. Tusichoke kusubiri. Bila kujali itachukua muda gani kuifikia.” Aliongeza mama yake na kumfuta machozi mtoto wake aliyekua kasimama pembeni ya kitanda.
“ila kwanini mama hauwi mkweli katika mambo yako na kila siku unaamua kunificha. Hata kama umri wangu bado. Ila unatakiwa usinifiche kila kitu kinachonihusu. Kimfano, mpaka hivi sasa bado hujanipa jibu sahihi kuhusiana na baba yangu… kwanini?”aliuliza mtoto kwa uchungu. Si kwa mapenzi ya baba yake, ila kwa kuchukia kuona mama yake akipata tabu peke yake wakati baba yake yupo hai.
“sio kwamba sitaki kuku eleza mwanangu. Ila muda bado hujafika. Ila nakuahidi kua. Pindi utakapo timiza miaka kumi. Basi nitakuambia kila kitu kuhusiana na maisha yangu.” Aliongea mama yake na kumshika kichwani mtoto wake huyo aliyekua mtiifu kuliko utiifu wenyewe.
“nimekuelewa mama. Ila kama ingetokea bahati mbaya umepoteza maisha, unafikiri ni nani angeweza kuni dadavulia siri uliyoiweka mchagoni mwa moyo wako?,. kumbuka mama. Mimi sihitaji kwenda kwa baba yangu hata siku moja. Ila kumjua ni jambo zuri. Au unaona nina kukosea nikimuulizia?” aliuliza mttoto swali lililomfanya mama yake atoe tena machozi.
“nakuomba mwanangu usinikumbushe machungu ya nyuma kabla sijaamua kukuelezea mwenye we kwa ridhaa yangu. Nakuomba badilisha mada hiyo mwanangu.” Aliongea mama huyo huku machozi yanamtoka. Hapo ndipo Yule mtoto alipojiona mkosaji na kuamua kutumia shati lake na kumfuta mama yake machozi.
“nisamehe mama, sio kusudio langu kukuliza mama yangu. Sitakuuliza tena mama…. Nyamaza kulia mama. Siku ya harusi yangu utalia nini?”
Aliongea Yule mtoto huku machozi yanamtoka . Maneno ya harusi yangu utalia lini, yalimfanya mama yake ajitahidi kunyanyuka na kumkumbatia.
Anayakumbuka sana hayo maneno matamu aliyoambiwa na mwanaume aliyebadilisha maisha yake kipindi ambapo alikua msichana mbichi kabisa tena akiwa bado hajalijua jiji vizuri. Sasa hivi amepitia hatua mbaya ambazo anaamini hakuna mtu ambaye angeweza kuvumilia kama angezipia hatua hizo.
Moyo ulimuuma na kumuangalia motto wake mdogo sana huku akimfuta machozi yaliyokua yakitiriririka bila kikomo kwenye mashavu yake.
“nakupenda sana mama… wewe ndio furaha yangu pakee.” Aliongea mtoto huku akimfuta machozi mama yake.
“sitalia tena…nitakuja kulia siku utakayooa mwanangu. Tena si kwa uchungu wa maumivu… bali kwa uchungu wa kutimiza ndoto za baba yako mlaghai.” Aliongea maneno hayo na kumkumbatia tena motto wake aliyemfariji kwa kumpapasa mgongoni.
ITAENDELEA ………………
TAFADHARI NAOMBA USIIKOPY NA KUIBADILISHA KITU CHOCHOTE .
Hello, nimependa na wewe mwenzangu usome hadithi hii nzuri. Utafurahi naamini. Ili usipitwe na hadithi tamu na nzuri nyingi kama hizi, unaweda download Hadithi App kutoka PlayStore kwa kubonyeza hapa: https://play.google.com/store/apps/details?id=com.developict.hadithi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon