Makonda awakabidhi rungu FFU kudhibiti UKUTA


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewapa rungu askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) mkoani hapa kuwadhibiti watakaothubutu kufanya maandamano ya kuunga mkono operesheni ya Chadema iliyopewa jina la Umoja wa Kupambana na Udikteta Tanzania (Ukuta).

Chadema walizindua operesheni hiyo na kutoa maazimio matatu ambayo yatatekelezwa  nchi nzima ikiwamo mikutano ya hadhara ambayo itafanyika Septemba Mosi, mwaka huu.

Wanadai wanataka kuzuia matukio ya ukandamizaji wa haki na demokrasia nchini inayofanywa na Rais, John Magufuli. Akizungumza jijini Dar es Salaam baada ya kukitembelea kikosi cha FFU Ukonga jana,  Makonda aliwataka askari wajipange kudhibiti Ukuta na hawana haja ya kusubiri maagizo kutoka kwa kiongozi yeyote.

Mwenyekiti mtatani kwa kumpa ujauzito mwanafunzi

POLISI mkoani Mwanza inamshikilia Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Sangabuye, Kata ya Igombe katika Manispaa ya Ilemela, John Mayala (38) akituhumiwa kumpa ujauzito na kumtorosha na mwanafunzi wa kidato cha pili (jina linahifadhiwa) wa Shule ya Sekondari ya Sangabuye.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi alisema jana kuwa mtuhumiwa anatuhumiwa kutenda kosa hilo Agosti 3, mwaka huu katika mtaa huo.
Aliongeza kuwa Polisi inamshikilia pia

Kategori

Kategori