Kanye West akutana na Donald Trump New York

Mwanamuziki mashuhuri nchini Marekani Kanye West, ambaye majuzi alilazwa hospitalini baada
ya kutatizwa na msongo wa mawazo na uchovu, amekutana na rais mteule wa Marekani Donald Trump jijini New York.
Bw Trump anasema wawili hao walizungumza kuhusu "maisha" kabla ya kupigwa picha pamoja.
Alisema wawili hao ni "marafiki" na akamweleza Kanye kuwa "mtu mzuri" lakini hakusema iwapo mwanamuziki huyo atatumbuiza wakati wa sherehe ya kuapishwa kwake mwezi Januari.
Kanye alisalia kimya alipokuwa na mwanachama huyo wa Republican.
Aliwaambia wanahabari: "Nataka tu kupigwa picha kwa sasa."
Taarifa kutoka Marekani zinasema Bw Trump huenda anakabiliwa na tatizo katika kutafuta wanamuziki mashuhuri wa kutumbuiza siku ya kuapishwa kwake.


EmoticonEmoticon