Mimba ya Jokate yadaiwa kuchoropoka
Mwanamitindo maarufu Bongo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’
IMEFICHUKA! Ile mimba ya mwanamitindo maarufu Bongo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ iliyokuwa ikisemekana ni ya Mbongo-Fleva, Ali Saleh Kiba inadaiwa kuharibika kwa kuchoropoka kisa kikiwa ni mazoezi makali aliyoyafanya hivi karibuni.
Kidoti na Ali Kiba
Chanzo makini kililiambia gazeti hili kwamba, Jokate kwa sasa hana ujauzito tena kwani ulichoropoka kufuatia mazoezi makali ya kujiandaa na shoo aliyofanya ya Nyama Choma Festival kwenye Viwanja vya Leaders Club Kinondoni jijini Dar iliyosapotiwa na mpenzi wake huyo.
“Kama mlikuwa hamjui kitumbo cha Jojo (Jokate) kilichoropoka kutokana na mazoezi makali ya shoo aliyoifanya hivi karibuni ambapo kwa sasa anaendelea vizuri na anafanya kazi zake kama kawaida bila ujauzito,” kilinyetisha chanzo hicho.
Baada ya kupata habari hizo, paparazi wetu alimtafuta Jokate na kumuuliza kuhusu ujauzito wake ambapo alijibu kwa ufupi: “Kwa sasa mimi sina mimba.”
Hata hivyo, chanzo hicho kiliendelea kueleza kwamba, kwa sasa Kiba anajipanga upya katika masuala hayo ya