DIAMOND PLATINUM AMKUMBUSHA RAISI KUHUSU UKUMBI.....

DIAMOND AMKUMBUSHA RAIS MAGUFULI
The perfect
Msanii mahiri nchini anaeipeperusha vyema bendera ya Tanzania nje ya nchi Nassib Abdul maarufu kama Diamond Plutnumz, amemkumbusha Rais Magufuli kuhusu ahadi yake ya

YAJUE MADHARA YA KUTOA MIMBA

HAYA NDIO MADHARA SITA YA KUTOA MIMBA…

Kutoa mimba ni nini? Hii ni hali ya mwanamke kwa hiari yake mwenyewe kuharibu mimba iliyoingia ndani ya kizazi chake.

Kutokana kuongezeka kwa idadi ya mahusiano duniani na kutotumia njia za uzazi wa mpango kwa watu wengi walioko kwenye mahusiano, wasichana wengi kwa sasa wanatoa mimba.
Utafiti nilioufanya mwenyewe nimegundua kwamba zaidi ya asilimia tisini ya wasichana wanaokua kwenye mahusiano na wanaume zaidi ya mwaka mmoja kabla ya ndoa hutoa mimba na asilimia tano tu ya wote ndio wanaamua kuzaa. Sio ajabu kusikia mtu ameolewa akiwa ametoa mimba nne mpaka tano. Sasa unajiuliza bado kuna mtu humo au mfu?

Hata hivyo hao wanaozaa pia hujikuta wamebeba mimba zingine wakati watoto wao wakiwa wadogo na kulazimika kuzitoa. Najua watu wengi wanatoa mimba kukwepa aibu, kutokua tayari kisaikolojia na kadhalika lakini ni bora kutumia njia za uzazi wa mpango kama condomu kuzuia mimba na kama kondomu huiwezi basi tumia njia zingine kama sindano na vijiti kwasababu wengi wenu mkishalewa pombe au kondomu isipokuepo ndio basi tena.

Hebu tuyaangalie madhara ya kutoa mimba kama ifuatavyo…

1. Uwezekano mkubwa wa kufa:
Utafiti uliofanywa na madaktari wa finland mwaka 1997 umegundua kwamba wanawake wanaotoa mimba wanauwezekano wa kufa mara nne zaidi kuliko ambao hawatoi mimba. Vifo hivyo vimekua vikisababishwa na kujiua wenyewe kutokana na kujuta kwa maamuzi yao na madhara ya mda mrefu ya kimwili yatokanayo na kutoa mimba. Vifo ndani ya wiki moja baada ya kutoa mimba hutokana na kuvuja damu sana, madhara ya dawa za usingizi, mabonge ya damu kwenye mishipa ya damu na mimba iliyotunga nje ya uzazi. Utafiti pia uliongeza kutoa mimba moja uwezekano wa kufa unakua 45%, mimba mbili 114%, mimba tatu 192%.

2. Ugumba kwa wanawake wengi:
Miaka hii ya karibuni wanawake wengi ambao wanalia kutopata watoto wana historia za kutoa mimba miaka iliyopita, na wengi wao nilionana nao wanajuta sana kwa maamuzi yao. Hii inatokana na madhara makubwa waliyoyapata kwenye mfuko wa uzazi baada ya mimba kutoka.

3.Mimba kutunga nje ya kizazi:
Mfuko wa uzazi una utando maalumu amaboa hufanya mimba iliyotungwa kwenye mirija iitwayo fallopian kuwezesha yai kushuka hadi kwenye mifuko ya uzazi. Lakini utoaji wa mimba huambatana na magonjwa ya mirija hiyo na kupoteza utando huo na kusababisha mimba kukulia huko.matibabu ya tatizo hili ni kukata mrija husika tu hivyo kuongeza hatari ya ugumba..

4.Kuzaa watoto wasio na akili nzuri:
Utoaji wa mimba kuharibu mlango wa mfuko uzazi kushindwa kushika vizuri na matokeo yake mwanamke huyu hujikuta akizaa kabla ya mda husika akibeba mimba nyingine. Lakini pia watoto hawa wanaozaliwa kabla ya muda maalumu  na viungo ambavyo havijakomaa hupata shida ya ubongo na kua wagonjwa wa akili maisha yao yote.

5.kansa ya mlango wa uzazi
Wanawake wanaotoa mimba wana hatari kubwa ya kupata kansa ya mlango wa uzazi kuliko wengine ambao hawajatoa mimba. Hii ni kwasababu ya kusumbuliwa kwa mlango huo kwa dawa za kutoa mimba, vifaa vya kutoa mimba na mabadiliko ya ghafla ya homoni za uzazi.

6.Kuathirika kisaikolojia;
Hakuna mwanamke ambaye hatakaa ajutie maamuzi yake ya kutoa mimba siku za usoni hata kama hakupata madhara yeyote hii itamfanya aishi kama ana deni Fulani maisha yake yote na itakua inamuumiza usiku na mchana. Zingine ni kukosa hamu ya kula, kusikia sauti ya mtoto anayelia wakati hayupo, kua na hasira sana…

Mwisho
kumbuka kila mwaka wanawake 70000 wanakufa kwa kutoa mimba...maumivu ya kukosa mtoto ni makali sana kuliko aibu ya kuzaa nje ya ndoa. Hawa wanaozaa sasa hivi unawaona malaya ipo siku utawakumbuka utakapo ambiwa na daktari kwamba labda itokee miujiza ndo utazaa.Kama hutaki mimba tumia njia za uzazi wa mpango kwani kuendelea kutoa mimba kutakupa adhabu ya kukosa mtoto ambayo adhabu hiyo utaitumikia maisha yako yote..

MARUFUKU KUCHEZA POOLTABLE ASUBUHI UKIKUTWA FAIN SH 300,000

Faini Sh300,000 kucheza pool tableasubuhi


Dar es Salaam. Wapenzi wa mchezo wa pool table nchini, watalazimika kusubiri hadi saa 10 jioni kucheza mchezo huo au kukubali kutozwa faini isiyopungua Sh300,000 wakikutwa wanacheza kabla ya muda uliopangwa.

Mkurugenzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Abbas Tarimba amesema wametayarisha barua zitakazotumwa kwa wakuu wa mikoa ili kuwasaidia kuelekeza wananchi kuhusu kanuni, sheria na taratibu za mchezo huo.

Alisema barua hizo pamoja na matangazo yatakayotoka katika vyombo vya habari, vitatoa mwongozo wa muda wa kuanza mchezo huo ambao utakuwa ni saa 10.00 jioni na kumaliza saa 5.00 usiku kwa siku za kazi, huku siku za mapumziko utaanza saa 8.00 mchana na kumalizika saa 6.00 usiku.

Tarimba alisema Sheria ya Michezo ya Kubahatisha (Gaming Act), kifungu cha 52 katika kifungu kidogo cha kwanza sura ya 42, inaeleza asiye na kibali cha kuchezesha au atakayekiuka kanuni za mchezo huo, atashtakiwa na akikutwa na hatia atalazimika kulipa faini isiyopungua Sh300,000 au kifungo kisichopungua miezi mitatu au vyote viwili.

“Kila shughuli hapa nchini ina taratibu zake, watakaokiuka kwa kisingizio cha kuwa hiyo ndiyo ajira yao, watakaokutwa wanautumia mchezo huo kinyume cha sheria na kuugeuza kamari, watachukuliwa hatua za kinidhamu,”alisema.

Wakati Tarimba akisema hayo kuunga mkono kauli ya Rais John Magufuli ya kupiga marufuku vijana kuucheza mchezo huo muda wa kazi, katika baadhi ya maeneo jijini Dar es Salaam bado unaendelea kuchezwa.

Mwananchi lilifanya uchunguzi katika maeneo ya Buguruni, Mabibo, Vingunguti na Ilala na kukuta vijana wakiendelea kucheza mchezo huo asubuhi, huku baadhi yao wakidai hawajui kama imepigwa marufuku.

Teophili Lyaka aliyekutwa akicheza katika baraza ya nyumba eneo la Mabibo, alisema hajui kama kuna katazo la kucheza mchana na pia analipa fedha mwenyewe na hana kazi ya kufanya.

Leonard Rupia aliyekutwa akicheza katika eneo la Ilala, alisema anatambua Rais amekataza na kusema watu wafanye kazi, lakini amesahau vijana wengi hawana kazi.

Alishauri kwamba vijana watafutiwe kazi kwanza kabla ya kulazimishwa kuacha kufanya vit vinavyowapotezea mawazo.

“Sijui hajui kama hatuna kazi, maisha magumu, mawazo kila kukicha,”alisema.

Cassian Gama anayechezesha mchezo huo eneo la Vingunguti, alisema hiyo ndiyo ajira yake na ametekeleza kilichokuwa kinasemwa na viongozi mbalimbali kuwa vijana watafute fursa za kujiajiri.

“Hapo awali nilikuwa naingiza hadi Sh100,000 kwa sababu ‘token’ ilikuwa inauzwa Sh500. Watu wakijaa wanaotaka kucheza haraka wanapanda dau hadi Sh1,000, lakini sasa yapo mengi. Nauza bei ya zamani na ninapata kati ya Sh20,000 hadi Sh22,000 ukiniambia niache unataka nifanye kazi gani,”alisema.

Miraji Ramadhani aliyekutwa akicheza eneo la Buguruni ambaye ni mchezeshaji pia, alisema hana mpango wa kuacha kucheza, kuchezesha hadi akamatwe ‘akapumzike’ kwa kuwa hana cha kufanya.    

MWANAMKE ALIYEOA WANAUME 2 AFARIKI DUNIA ?!!

Mwanamke Aliyeoa Wanaume wawili Afariki Dunia


MKAZI wa Kijiji cha Ikondamoyo, Wilaya ya Mlele mkoani Katavi, Veronica Salehe (54), aliyeoa wanaume wawili kwa kipindi cha miaka tisa amefariki dunia.

Akizungumza na waandishi wa habari juzi, Mwenyekiti wa Kitongoji cha Ikondamoyo, John Maganga, alisema Veronica alifariki dunia wiki iliyopita mkoani Tabora alikokuwa amekwenda  kupatiwa matibabu kwa kaka yake.

Maganga alisema kuwa ndoa hiyo iliwezeshwa na mume mkubwa ambaye alikubali kuishi na mume mdogo.

Alisema kuwa Veronica ndiye aliyewaoa wanaume wote wawili na kuishi nao kwa miaka tisa, na kwamba ndiye aliyekuwa na amri kuu katika nyumba yao.

Aliwataja wanaume hao kuwa ni Paulo Sabuni (62) ambaye ndiye mume mkubwa na Arcado Mlele (47).

Maganga alisema Veronica na mume wake mkubwa, walifika kijijini hapo miaka 24 iliyopita wakitokea Kijiji cha Usumbwa, mpakani mwa Chunya na Tabora.

“Baada ya kufika kijijini hapa, walianza kujishughulisha na shughuli za kilimo na biashara ya kuuza pombe za kienyeji aina ya komoni,” alisema Maganga.

Katika uhai wake, Veronica alibahatika kupata watoto wanne, kati yao wawili wa kike.

Maganga alisema mtoto mdogo wa kiume, ni wa mume mdogo ambaye ana miaka tisa, anayesoma darasa la nne katika Shule ya Msingi Ikondamoyo, na watoto wengine watatu ni wa mume mkubwa.

Kuhusu maisha ya Veronica ya kuishi na wanaume wawili, Maganga alisema haikuwa siri kijijini hapo kwa sababu walizoeleka kwa wanakijiji.

Alisema mume mdogo alikuwa anaishi kwenye nyumba aliyoachiwa na marehemu baba yake, lakini alikuwa akishinda kwa mume mkubwa ambako kulijulikana zaidi kwa jina la ‘nyumba kubwa’.

“Mambo ya kula, kunywa na mengine, mama   alikuwa akiwapangia zamu kama afanyavyo mume mwenye wake wengi,” alisema Maganga na kuongeza kuwa wanaume hao walikuwa wanaridhika na kufurahia maisha.

Alisema siku mama akichoka kupika, mume mdogo alikuwa akiingia jikoni na kuwaandalia chakula watoto na mume mkubwa maji ya kuoga.

Wakati wa mazishi, wanaume wote walishiriki shughuli zote, jambo ambalo limeacha maswali mengi kwa jamii.

Akizungumzia msiba huo, mume mkubwa alisema kuwa amepata pigo kubwa kwa sababu alikuwa anasaidiwa mno na marehemu Veronica kutokana na biashara zake za pombe za kienyeji ambazo zilisaidia kuendesha maisha ya kila siku.

“Veronica aliugua muda wa miezi miwili, nilikuwa namplekea Kituo cha Afya Urwila kupata matibabu, lakini Mungu kampenda zaidi,” alisema.

Kategori

Kategori