Papa kutua Kenya Kesho.
Nairobi, Kenya. Kiongozi wa Kanisa Katoliki Papa Francis amesema kwamba kesho akiwa Kenya atatoa ujumbe wa amani.
Kiongozi huyo Katika taarifa aliyoituma juzi, alitoa wito kwa
waandaaji wa ziara yake wakumbuke kuomba ili
ziara hiyo ilete matumaini kila mmoja.
ziara hiyo ilete matumaini kila mmoja.
Utafiti uliofanywa na kampuni ya Infotrak mwishoni mwa wiki
ulionyesha kuwa asilimia 93 ya raia wa Kenya wana hamu ya ziara ya
kiongozi huyo wa kanisa Katoliki ulimwenguni.
“Wakenya wengi wanatarajia kujitokeza mapokezi ziara ya Papa kesho.
Matarajio hayo yako kwa Wakenya wote bila kujali dini wala kabila,”
alisema Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Infotrak Angela Ambitho.
Alisema raia wa nchi hiyo 777 walihusishwa katika utafiti huo
uliofanywa Ijumaa. Asilimia 98 ya Wakatoliki wanafurahia ziara ya Papa
Francis na asilimia 91 ya Wakenya wa madhehebu na dini zingine walisema
wanamkaribisha Kenya.
Utafiti huo ulionyesha kuwa Papa Francis anayefanya ziara yake ya
kwanza Afrika anapendwa na Wakenya wote Wakatoliki na wasio Wakatoliki.
“Papa Francis anapendwa na Wakatoliki ambao wamekumbatia unyenyekevu wake na wito wa kushirikisha wote,” alisema Ambitho.
“Kupendwa kwa Papa kunaonekana kupiku Kanisa Katoliki ambalo licha ya
kukumbwa na kashfa mbalimbali ulimwenguni lina wafuasi wengi Kenya,”
aliongeza
Mabadiliko
Kwa mujibu wa utafiti huo, asilimia 95 ya Wakatoliki nchini Kenya wanahisi Papa Francis ataleta mabadiliko katika kanisa hilo.
Aidha, asilimia 98 ya Wakatoliki Kenya wanahisi kwamba Papa Francis
ataleta mabadiliko mazuri katika dini ya Kikristo, asilimia 85 ya
Wakenya wa madhehebu mengine wanahisi kwamba ataleta mabadiliko katika
dini
EmoticonEmoticon