MHUBIRI MAARUFU DUNIA TB JOSHUA KUTOKA NIGERIA AWASILI TANZANIA>> KUSHUHUDIA KUAPISHWA KWA MH. JOHN POMBE MAGUFULI

Mhubiri maarufu duniani  TB Joshua wa kanisa la Church of All Nations nchini Nigeria  ametua jijini Dar es salaam tayari kwa kushuhudia kuapishwa kwa Rais wa Awamu ya Tano Dkt. John Pombe Magufuli siku ya Alhamisi.Novemba 5,2015
Mara tu baada ya kutua uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, TB Joshua alikwenda
Ikulu moja kwa moja kumsalimia Rais Jakaya Mrisho  Kikwete  kumsabahi na kumpongeza kwa kufanikisha uchaguzi mkuu kwa uhuru na amani, huku akiondoka madarakani akiwa mtu mwenye furaha. TB Joshua amepongeza Rais Kikwete pia kwa kupata Dkt Magufuli kama mrithi wake, akimtaja Rais huyo mpya mteule kama Rais wa Tanzania wa Baraka na Fanaka tele katika awamu hii mpya.

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimlaki Mhubiri  TB Joshua wa kanisa la Church of All Nations la nchini Nigeria Ikulu jijini Dar es salaam TB Joshua ametua jijini Dar es salaam  tayari kwa kushuhudia kuapishwa kwa Rais wa Awamu ya Tano Dkt. John Pombe Magufuli siku ya Alhamisi.

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mhubiri  TB Joshua wa kanisa la Church of All Nations la nchini Nigeria Ikulu jijini Dar es salaam 



.        

Related Posts


EmoticonEmoticon

:)
:(
=(
^_^
:D
=D
=)D
|o|
@@,
;)
:-bd
:-d
:p
:ng
:lv