Mawaziri watano wa serikali
inayomaliza muda wake wameanguka kwenye uchaguzi katika majimbo yao,huku
wagombea wengine wa Ubunge maarufu nao wakiangushwa na Kambi ya
upinzania katika matokeo ya kura yanayoendelea kutolewa kufuatia
uchaguzi mkuu wa nchini humo uliofanyika Jumapili.
Mawaziri hao watano wa serikali ya Jakaya Mrisho Kikwete
inayomaliza muda wake ni
1.Stephen Wassira Waziri wa Kilimo Chakula na
Ushirika
2. Dk Steven Kebwe,Naibu Waziri wa Afya
,3.Christopher Chiza Waziri
wa Nchi,Ofisi yaRais,Uwekezaji na Uwezeshaji,
4.Anne Kilango
Malecela,Naibu Waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi na
5. Omar Nundu
aliyewahi kuwa Waziri wa Uchukuzi.
Mawaziri hao walioangushwa
katika majimbo yao wanaungana na wabunge wengine maarufu katika Bunge la
Kumi la Tanzania waliong'ara ambao kwa sasa wameshindwa kurejea.
Hata
hivyo pia wamo mawaziri wa Zamani Cyril Chami na Omary Nundu.Tume ya
taifa ya Tanzania inaendelea kutangaza matokeo ya Ubunge na Urais.
EmoticonEmoticon