Showing posts with label ELIMU. Show all posts
Showing posts with label ELIMU. Show all posts
TCU YAFUNGIA VYUO VINGINE KUDAHILI.

TCU YAFUNGIA VYUO VINGINE KUDAHILI.

TCU YAFUNGIA VYUO VINGINE KUDAHILI.

BAADA ya wiki jana kutangaza orodha ya vyuo ambavyo havitaruhusiwa kudahili Wanafunzi Kwa Mwaka wa Masomo 2016/17, leo Tume hiyo imetoa orodha nyingine ya vyuo ambavyo vimefungiwa kufanya udahili kutokana na sababu mbalimbali. Vyuo vilivyozuiwa kudahili ni pamoja
na;

1. Katavi University of Agriculture - Kozi zote.

2. Ekernforde Tanga University - Kozi zote.

3. Hubert Kairuki Memorial University - Kozi ya udaktari.

4. Muslim University of Morogoro - Kozi ya uandishi wa habari na mawasiliano ya umma.

5. St. Joseph University In Tanzania (St.Mark's University College) - Kozi zote.

6. United African University of Tanzania - Kozi zote.

7. Tanzania International University - Kozi zote.

8. Kampala International University, Dar es Salaam College - Kozi ya Sayansi ya Kompyuta.

9. St. Joseph University College of Management and Commerce - Kozi zote.

10. Tumaini University, Dar es Salaam College - Kozi ya uandishi wa habari na mawasiliano ya umma.

12. Stefano Moshi Memorial University College - Kozi zote.

13. Teofilo Kisanji University, Tabora campus - Kozi zote.

14. University of Arusha, Musoma campus - Kozi zote.

15. Mount Meru University, Mwanza campus - Kozi zote.

16. University of Mbeya - Kozi zote.

17. Mzumbe University, Mwanza campus - Kozi zote.

18. Stella Maris Mtwara University College - Kozi zote.

19. ArchBishop James University College - Kozi zote.

20. Mwalimu Julius K. Nyerere University of Science and Technology - Kozi zote.

21. Josiah Kibira University College - Kozi zote.

22. College of Business Education, Mwanza campus - Kozi zote za shahada na shahada na Shahada ya Uzamili.

Kwa taarifa zaidi tembelea http://www.tcu.go.tz


Wanafunzi wa awamu ya pili waliopangiwa mikopo -2015/2016

Awamu ya Pili ya Wanafunzi waliopangiwa Mikopo - 2015/16

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
AWAMU YA PILI YA WANAFUNZI WALIOPANGIWA MIKOPO KWA 2015/2016_Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) inapenda kuwafahamisha waombaji wa mikopo kwa mwaka wa masomo 2015/2016 kuwa imetoa Awamu ya Pili ya waombaji 28,554 waliofanikiwa kupata mikopo na kufanya idadi ya waombaji wenye sifa wa mwaka wa kwanza waliofanikiwa kupata mikopo hadi sasa kufikia 40,836.
Katika awamu ya kwanza, Bodi ilitoa orodha yenye jumla ya waombaji 12,282 waliofanikiwa kupata mikopo.
Majina ya waombaji waliofanikiwa kupata mikopo kutoka katika awamu zote mbili yanapatikana kupitia mtandao wa Bodi waolas.heslb.go.tz na tovuti ya Bodi (Bofya Hapa www.heslb.go.tz ) Aidha, orodha hizo pia zimetumwa vyuoni kwa ajili ya taratibu za usajili.
Lengo la Bodi ni kuhakikisha kuwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza wenye sifa ya kupata mikopo katika mwaka wa masomo 2015/2016 wanapata mikopo na hivyo kupata elimu ya juu.
Aidha, Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inapenda kuwasihi waombaji wa mikopo kuwa watulivu na kupuuza taarifa zinazosambaa katika baadhi ya mitandao ya kijamii kuwa Bodi haitatoa mikopo kwa waombaji kwa mwaka wa masomo 2015/2016.
       
Imetolewa na:
MKURUGENZI MTENDAJI
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU

Kategori

Kategori