Tumbo la zari lashangaza wengi mwenyewe asema hivi

ZARI Awashangaza Wengi Baada ya Tumbo lake la Uzazi Kupungua Ndani ya Wiki Moja...Atoa Ushauri Huu
USHAURI WA ZARI KWA WAZAZI from #zarithebosslady - Good morning.... ladies no need to worry coz our bodies are different. But I did exercise during pregnancy which has helped my body get bk within 7days.... and for those stretch marks keep using olive oil during and after pregnancy.

Bifu la Akikiba Na Dull sykes

BIFU la Alikiba na Dully Sykes...Alikiba Afunguka Haya
Mkali wa wimbo Aje Alikiba baada ya kuondoka na tuzo tatu za EATV, amefunguka na kuzungumzia mahusiano yake na msanii mkongwe wa muziki na producer, Dully Sykes. Hatua hiyo imekuja kutokana na kuenea kwa taarifa za muda mrefu katika mitandao ya kijamii kwamba wawili hao hawaelewani. Katika usiku wa tuzo za EATV, Dully ndiye aliyemtangaza mshindi wa video bora ya mwaka Alikiba kupitia video yake ya wimbo ‘Aje’ kabla ya kukabidhiwa tuzo na Katibu Mkuu wa Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) Godfrey Mngereza. Akiongea muda mfupi baada ya kuchukua tuzo hiyo akiwa pamoja na Dully Sykes, Alikiba alizishukuru tuzo hizo kwa kumkutanishwa na Dully Sykes huku akidai yeye anamchukulia kama baba katika muziki. “Mwenyezi Mungu leo ametukutanisha, huyu mimi ndiye aliyenianzisha, huyu ndiye aliyenifanya niamini mimi najua kuimba, nilichokuwa nikiimba brother Dully Sykes muda mwingine nilikuwa namtoa mpaka machozi,” Ali alikiambia kipindi cha Enewz cha EATV akiwa mbele ya Dully Sykes. “Nisipotokea siku mbili hata siku moja kwao lazima ataniulizia Ali yupo wapi. Sina simu sina nini, Dully Sykes alikuwa ananipenda sana sijajua sasa hivi lakini mimi kwangu Dully ni brother wangu na ninaweza nikamuita baba yangu wa kimuziki wa bongofleva. Mimi sina mengi ya kusema ila nataka ajue kwama mimi nampenda siku zote na nitampenda mpaka nakufa,” Naye Dully Sykes baada ya kusikia kauli hiyo ya Alikiba na yeye alisema hana tatizo na muimbaji huyo wa Aje na kusema anampenda pia.

DARASA AMKUNA PROFESA J

PROFESA Jay Akunwa Kisawa Sawa na Mwanamuziki Darasa Atoa ya Moyoni
Mafanikio ya Mwanamuziki Darasa kwenye muziki yamemfanya Prof Jay Kusema haya Kupitia mtandao wa Instagram, Jay ameandika: Mdogo wangu @darassacmg Imani yako, Kutokukata tamaa na Struggle yako ya Usiku na Mchana ndio imekufanya ufikie hapo ulipofikia, Nakumbuka wakati unashoot Wimbo wako wa USIKATE TAMAA uliniambia unatamani ufikie level za juu kama zetu, Nami nilikwambia hakuna kinachoshindikana chini ya JUA Ukiset GOALS, kufanya kazi kwa bidii na SALA yote Yanawezekana, Naamini kwa style hii ya JIWE juu Ya JIWE, NDOTO yako inakwenda kuwa kweli, Cha MSINGI usiridhike na mafanikio haya..HUU ni mwanzo tuu na mafanikio makubwa zaidi yako at your DOOR, Keep your eyes open and Keep ya HEAD UP, SKY IS THE LIMIT, GO GET DEM… BLESS #ACHA MANENO WEKA MUZIKI

Kamanda Sirro: Asema Aliyetishwa na kauli ya Mzee wa Upako afungue kesi

Kamanda Sirro: Aliyetishwa na kauli ya Mzee wa Upako afungue kesi
 Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam imemtaka yeyote anayeona kuwa kauli iliyotolewa na Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo maarufu Mzee wa Upako imetishia maisha yake, afungue kesi. Kamanda wa kanda hiyo, Simon Sirro aliyasema hayo jana Dar es Salaam wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari waliotaka kujua hatua polisi waliyoichukua kutokana na kauli aliyoitoa Mchungaji huyo kwamba waandishi waliomwandika vibaya watakufa kabla ya Machi mwakani. “Kama kuna mtu anaona katishika na kauli hiyo aje afungue kesi milango iko wazi. Kama kuna mwandishi yeyote anayeona ametishika na kauli hiyo aje, kesi ikifunguliwa tutaifanyia kazi kwa sababu hadi sasa hakuna aliyelalamika,” alisema. Kauli ya Mzee wa Upako aliitoa katika mahubiri yake ya Jumapili ikiwa ni mwendelezo wa majibu yake kutokana na tuhuma zilizoandikwa kwenye baadhi ya vyombo vya habari kwamba alimfanyia fujo jirani yake. Wakati huo huo, Sirro alisema kuwa wanaendelea na uchunguzi wa madai ya kupotea kwa Bernard Saanane ambaye ni kiongozi wa Chadema. Kiongozi huyo anadaiwa kupotea tangu Novemba 18. “Kuna watu wanasema wanataka ile miili ichunguzwe… lile ni tukio la Pwani na mwenye wasiwasi anaruhusiwa kuwasiliana na uongozi wa kule kwa sababu ule ni mkoa mwingine,” alisema. Hata hivyo, alipoulizwa kuhusu kukamatwa kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Forum, Maxence Melo alisema atazungumzia suala hilo Ijumaa.

Salamu zisizokuwa za kawaida nchini Cameroon watu wanapost picha zao

Tangu waziri wa michezo nchini Cameroon Pierre Ismael Bidoung Mpkatt ainame wakati akimsalimia rais wa nchi hiyo Paul Biya, picha hizo zilisambaa mitandaoni.
Watu nchini Cameroon wamekuwa wakiiga picha hizo na hata kuifanyia mabadiliko




Kanye West akutana na Donald Trump New York

Mwanamuziki mashuhuri nchini Marekani Kanye West, ambaye majuzi alilazwa hospitalini baada
Maamuzi ya Halmashauri kuu ya Taifa ya CCM

Maamuzi ya Halmashauri kuu ya Taifa ya CCM

Haya Ndiyo Maamuzi Ya Halmashauri Kuu Ya Taifa Ya CCM Baada Ya Kikao Chake   Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM imekutana jana tarehe 13/12/2016 jijini Dar es salaam kwa kikao cha siku moja cha kawaida. Kikao hicho kimeongozwa na Mwenyekiti wa Taifa wa CCM Dkt. John Pombe Magufuli. Pamoja na mambo mengine, Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM imepokea taarifa ya Tathimini ya Uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, baada ya kuitafakari taarifa hiyo, Halmashauri Kuu imeamua yafuatayo;- 1. Kupunguza idadi ya wajumbe wa vikao na idadi ya vikao vya Chama katika ngazi mbalimbali ili kuongeza ufanisi wa utendaji wa Chama na kuongeza muda wa viongozi wa Chama kufanya kazi za Chama kwa Umma badala ya kutumia muda mwingi vikaoni. Ili kuwa na vikao vya Chama vyenye tija imeamuliwa kama ifuatavyo:- a). Halmashauri Kuu ya Taifa kwa sasa ina jumla ya wajumbe 388 idadi ambayo ni kubwa sana, hivyo imeamuliwa idadi hii ipunguzwe na kuwa wajumbe 158 kama ifuatavyo:- Wenyeviti wa Mikoa Mikoa ya Bara 26x1 = 26 Mikoa ya Zanzibar 6x1 = 6 Wajumbe wa NEC wa Mikoa Mikoa ya Bara 26x1 = 26 Mikoa ya Zanzibar 6x4 = 24 Wajumbe wa NEC wa Taifa Kutoka Bara = 15 Kutoka Zanzibar = 15 Nafasi za Mwenyekiti = 7 Wajumbe wa NEC wa Jumuiya UVCCM = 5 UWT = 5 WAZAZI = 5 Wajumbe wa NEC kutoka Bungeni = 5 Katibu wa Kamati ya Wabunge wa CCM = 1 Wajumbe wa NEC kutoka BLW = 3 Katibu wa Kamati ya Wawakilishi = 1 Wajumbe wa NEC – wanaotokana na Nyadhifa zao - Mwenyekiti wa CCM = 1 - Makamu Mwenyekiti (B) = 1 -Makamu Mwenyekiti (Z) = 1 - Makamu wa Rais = 1 - Waziri Mkuu = 1 - Makamu wa Pili wa Rais (Z) = 1 - Spika wa Bunge = 1 - Spika wa BLW = 1 - Mwenyekiti wa UWT = 1 - Mwenyekiti wa WAZAZI = 1 -Mwenyekiti wa UVCCM = 1 - Katibu Mkuu – WAZAZI = 1 - Katibu Mkuu – UWT = 1 - Katibu Mkuu – UVCCM = 1 Jumla: 158 #. Vikao vya kawaida vya Halmashauri Kuu ya Taifa vifanyike kila baada ya miezi sita badala ya miezi minne kama ilivyo sasa isipokuwa vinaweza kufanyika vikao maalum inapohitajika. b). Kwa upande wa sasa imeamuliwa wajumbe wa Kamati Kuu wawe 24 badala ya 34 kama ifuatavyo:- Mwenyekiti wa CCM. Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) Makamu wa Rais Katibu Mkuu wa CCM Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar) Waziri Mkuu Makamu wa Pili wa Rais (Z) Spika wa Bunge la Tanzania Spika wa BWL Mwenyekiti wa WAZAZI Mwenyekiti wa UWT Mwenyekiti wa UVCCM Katibu wa wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa Organaizesheni Katibu wa wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa Itikadi na Uenezi Katibu wa wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa Uchumi na Fedha Katibu wa wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Wajumbe watatu (3) wa kuchaguliwa na Halmashauri Kuu kutoka Tanzania Wajumbe watatu (3) wa kuchaguliwa na Halmashauri Kuu kutoka Zanzibar. #. Vikao vya kawaida vya Kamati Kuu vipunguzwe ili vifanyike kila baada ya miezi minne badala ya miezi miwili isipokuwa vinaweza kufanyika vikao maalum inapohitajika. c). Kwa ngazi ya mkoa, Wajumbe wa Kamati za Siasa za Mikoa wapunguzwe kwa kuondoa wajumbe watatu ambao ni:- Katibu wa Uchumi na Fedha wa Mkoa - 1 Wajumbe wa kuchaguliwa na H/Mkoa - 2 #. Vikao vya kawaida vya Kamati ya Siasa ya Mkoa vifanyike kila baada ya miezi mitatu badala ya kila mwezi kama ilivyo sasa isipokuwa vinaweza kufanyika vikao maalum inapohitajika. d). Kwa upande wa Wilaya Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Wilaya wapunguzwe kwa kuwoandoa:- Katibu wa Uchumi na Fedha wa Wilaya - 1 Katibu wa Kamati ya Madiwani - 1 Wajumbe wa kuchaguliwa na H/Kuu ya (W)- 2 Jumla: 4 #.Vikao vya kawaida vya Kamati ya Siasa ya Wilaya vifanyike kila baada ya miezi mitatu badala ya kila mwezi isipokuwa vinaweza kufanyika vikao maalum inapohitajika. #. Muundo wa Wilaya za Chama uendane na muundo wa sasa wa Serikali. Kata,Tawi na Shina Idadi ya kuanzisha Shina iwe wanachama 50 hadi 300. Idadi ya kuanzisha Tawi iwe wanachama kuanzia 301 hadi 1,000. Hata hivyo idadi hii izingatie eneo la kijiografia na wingi wa wanachama katika eneo hilo. Vikao vya kawaida vya Kamati za Siasa za ngazi hizi viwe vinafanyika mara moja kila baada ya miezi mitatu, isipokuwa vinaweza kufanyika vikao maalum inapohitajika. #. Nafasi za Uongozi Mwanachama anatakiwa kuwa na nafasi moja tu ya uongozi wa kazi za muda wote kama ilivyoainishwa kwenye Kanuni za uchaguzi wa Chama Toleo la 2012 kifungu cha 22 na 23 ambazo zimetajwa kuwa ni:- Mwenyekiti wa Tawi,Kijiji au Mitaa. Mwenyekiti wa Kata/Wadi. Mwenyekiti wa Jimbo, Wilaya na Mkoa. Makatibu wa Halmashauri Kuu wa ngazi zote zinazohusika. Mbunge, Mwakilishi na Diwani. #. Viongozi wa kuchaguliwa waepuke kuwa watendaji badala yake waongoze na kusimamia shughuli za Chama kwa kuzingatia Katiba na Kanuni. #.Vyeo ambavyo haviko kwenye Katiba Vyeo ambavyo havijatamkwa kwenye Katiba ya CCM haviruhusiwi katika Chama au Jumuiya zake mfano Umoja wa makundi mbalimbali kama Wenyeviti wa ngazi mbalimbali (mfano: Mwenyekiti wa Wenyeviti wa CCM n.k), Makamanda (UVCCM), Washauri (UWT) na Walezi (WAZAZI) katika ngazi zote. #. Uhakiki wa Wanachama wa CCM Halmashauri Kuu imeona ipo haja ya kufanya uhakiki wa wanachama wa CCM na Jumuiya zake ili kujua idadi sahihi ya wanachama wetu kwa wakati huu. Uhakiki huu uendane na kutoa kadi mpya za uanachama za kielektroniki ili kuwa na udhibiti wa usahihi wa wanachama na kuondoa wanachama HEWA. Aidha, Kadi za UWT, WAZAZI na UVCCM zifutwe ili tubaki na kadi za CCM tu. #. Jumuiya za Chama Cha Mapinduzi Jumuiya za CCM zimetakiwa kufanya kazi zake kwa kuzingatia matakwa ya Katiba ya CCM na Kanuni za Jumuiya husika, kanuni za Jumuiya ziendane na matakwa ya Katiba ya CCM. #.Uaendeshaji wa shughuli zote za Jumuiya za Chama na mali zake uwe chini ya usimamizi wa Chama Cha Mapinduzi. (Baraza la Wadhamini la Chama Cha Mapinduzi). Makatibu Wakuu wa Jumuiya watakuwa wanateuliwa na Kamati Kuu na Manaibu Katibu Wakuu watateuliwa na Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa. #. Wakati tukiendelea kubaki na Bendera yenye rangi ya kijani na njano na alama ya jembe na nyundo, Halmashauri Kuu imeona ipo haja ya kuzifanya rangi hizo kuwa na muenekano wa kuvutia zaidi. #. Utumishi katika Chama na Jumuiya zake. Katibu Mkuu wa CCM na Sekretarieti ipewe majukumu ya kusimamia ajira za Watumishi wa Chama na Jumuiya zake. Nafasi za Makatibu Wasaidizi wa Mikoa na Wilaya zitaondolewa na badala yake kazi zao zitatekelezwa na Makatibu wa Jumuiya za Chama wa Mikoa na Wilaya kwa utaratibu utakaopangwa. Utaratibu huu utakipunguzia Chama Cha Mapinduzi gharama na kujenga umoja wa utendaji kazi wa Chama na Jumuiya zake katika Mikoa na Wilaya. #. Tathimini ya hali ya Kisiasa na Uchaguzi wa Zanzibar . Halmashauri Kuu ya Taifa imeagiza kuundwa kwa Kamati maalum ya kufanya tathimini ya kina kuhusu hali ya kisiasa Zanzibar kwa ujumla na masuala yanayohusu uchaguzi wa Zanzibar 2015. # Mwenyekiti wa Kamati ya udhibiti na nidhamu ametakiwa akamilishe kazi ya taarifa ya udhibiti kwa wanachama waliokiuka mienendo ya kiuanachama kabla ya kuanza uchaguzi Mkuu wa Chama mwezi Februari 2017, Mikoa na Wilaya ambazo hazijaleta taarifa zao za kiudhibiti ziwe zimefikisha taarifa zao kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Udhibiti na Nidhamu kabla ya tarehe 30/01/2017. #. Uhakiki wa Mali za Chama uendelee kufanyika kwa kina na uchambuzi zaidi ukikamilika Taarifa yake iwasilishwe kwa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa mapema iwezekanavyo. #. Maamuzi na mapendekezo haya yatapelekea kufanyika kwa mabadiliko ya Katiba ya Chama na Kanuni za Jumuiya za Chama. #. Kwa mambo yale ambayo yatahitaji mabadiliko ya Katiba, Mkutano Mkuu utaandaliwa mapema mwakani na kutafakari na kupitisha mabadiliko hayo ya Katiba. Mwenyekiti wa CCM Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ameteua wafuatao kujaza nafasi mbalimbali ndani ya sekretarieti ambazo zimekuwa wazi kutokana na waliokuwa wakizishikilia kupewa majukumu mengine ya kiserikali. #.Ndg. Rodrick Mpogolo anakuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Ndg. Rajabu Luhwavi ambaye ameteuliwa kuwa balozi. #. Col. Ngemela Eslom Lubinga- Kuwa Katibu NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Dr. Asha-Rose Migiro aliyeteuliwa kuwa Balozi #. Humphrey Polepole kuwa Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Ndg. Nape Nnauye aliyeteuliwa kuwa Waziri. #. Wajumbe wengine watabaki kama walivyo sasa. Imetolewa na:- NAPE NNAUYE IDARA YA ITIKADI NA UENEZI 13/12/2016

Kategori

Kategori