HATIMAYE TUME YA UCHAGUZI YATANGAZA MSHINDI KATIKA uchaguzi wa urais Tanzania:DK. MAGUFULI ASHINDA>>>> SOMA ZAIDI UJUE KILICHOJILI

Magufuli atangazwa mshindi uchaguzi wa urais Tanzania

Mgombea wa urais kupitia tiketi ya chama cha
 CCM John Pombe Magufuli ndiye rais mteule
 wa taifa la Tanzania baada ya kushinda
 uchaguzi mkuu uliokamilika.
Akitoa matokeo hayo Mwenyekiti wa tume
hiyo jaji mstaafu Damian Lubuva amesema
 kuwa Magufuli alijipatia kura milioni 8,802,935
 ikiwa ni aslimia 58.46 huku mpinzani wake wa
karibu Edward Lowassa wa chama cha Chadema
 akijipatia kura milioni 6,072,848 ikiwa ni aslimia 39.97.
Haya ndiyo matokeo kamili kama yalivyotangazwa
 na mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi                                 
 Tanzania Jaji Mstaafu Damian Lubuva:

Matokeo ya uchaguzi wa urais Tanzania
Jina Chama Kura Asilimia
Anna Mghwira ACT 98,763 0.65
Chifu Yemba ADC 66,049 0.43
John Magufuli CCM 8,802,935 58.46
Edward Lowassa CHADEMA 6,072,848 39.97
Hashim Spunda CHAUMA 49,256 0.32
Janken Kasambala NRA 8,028 0.05
Macmillan Lyimo TLP 8,198 0.05
Fahmi Dovutwa UPDP 7,785 0.05    


EmoticonEmoticon