Kupatwa kwa jua 1 sep 2016

KATIKA GAZETI TANDO HILI UTAWEZA KUJIPATIA HABARI MOTO MOTO KATIKA PICHA ZA MATUKIO MBALIMBALI KUTOKA NDANI NA NJE YA TANZANIA HASA YALE YANAYOGUSA MAISHA YA KILA SIKU YA MTANZANIA.LUGHA KUU INAYOTUMIKA HUMU NI KISWAHILI.

June 22, 2016

JUA KUPATWA KIPETE MWEZI SEPTEMBA MOSI 2016

 Mtaalam wa Astronomia (Astronomy) kutoka Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) Dk. Noorali Jiwaji wa  Kitivo cha Sayansi, Teknologia na Elimu ya Mazingira, akizungumza na wanahabari (Hawapo pichani) wakati wa kuelezea tukio hilo  leo Juni 22.2016, Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu Mkuu wa chuo hicho kikuu Huria, Profesa Elifas Tozo Bisanda.

Mtaalam wa Astronomia (Astronomy) kutoka Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) Dk. Noorali Jiwaji wa  Kitivo cha Sayansi, Teknologia na Elimu ya Mazingira, akizungumza na wanahabari (Hawapo pichani) wakati wa kuelezea tukio hilo  leo Juni 22.2016, Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu Mkuu wa chuo hicho kikuu Huria, Profesa Elifas Tozo Bisanda.

 Muonekano endapo mtumiaji atatumia kichujia jua maalum.

Ramani ya Afrika inavyoonekana pindi tukio hilo litalavyokuwa…

Ramani ya Tanzania inavyoonesha itakavyokuwa siku tya tukio.

*************

TUKIO kubwa la angani la kipekee la kupatwa kwa jua usawa wa Tanzania litatokea Septemba 1, 2016, kuanzia saa 4:17 asubuhi hadi Saa 7:56 adhuhuri.

Washabiki na wanataaluma wa anga kutoka duniani kote pamoja na wanasansi, wanafunzi pamoja na jamii ya watanzania wataelekea Rujewa, kusini mwa Tanzania, Karibu na Mkoa wa Mbeya kushuhudia duara la jua linavyobadilika kuwa pete ya jua. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

Nchini kote Tanzania mamilioni ya watu watashangaa kuona jua kali la utosi likimegwa kwa zaidi ya asilimia 90 kwa kufunikwa na mwezi katika kupatwa kwa jua lionekane kama hilali nyembamba au kama mwezi mwandamo.

Katika tukio hili la kupatwa kwa jua, watu wanaoishi ndani ya ukanda wenye upana wa kilomita 100 unaokatisha Kusini ya Tanzania kutoka Congo kuelekea Katavi, mbeya, Ruvuma hadi Masasi na kuingia Msumbuji, siku hiyo jua kama duara jembamba kama pete kwa vile asilimia 98 ya jua litakuwa limejificha nyuma ya mwezi.

Kupatwa huko kwa jua kunaweza kuonekana kwa usalama na watazamaji, lakini inabidi kutumia vichuja maalum vya mwanga wa jua.

Tukio la kupatwa ni la kusisimua na la nadra sana kutokea katika maisha ya mtu. Hasa kwa kizazi hiki kipya ambacho kimechangamka kitasisimuliwa sana na tukio la ajabu kama hili na watajifunza Sayansi ili kuelewa kwa nini kinatokea kile wanachokiona.

Kwa hiyo tukio hili linaweza kutumiwa na shule na taasisi za elimu kuendeleza Sayansi na kuvuta wanafunzi kujiendeleza kisayansi na hasa kuelewa mizunguko mbalimbali iliyopo katika mfumo wetu wa sayansi pamoja na anga za juu kwa ujumla. Kuongeza uelewa wa sayansi ni muhimu katika kuelewa maumbile ya ulimwengu wetu.

Kupatwa huku kutatokea siku ya alhamisi ambapo wanafunzi wengi watakuwa mashuleni na ni wakati wa masomo.

Kwavile mchakato wote utaendelea kwa saa nne  hivi , kati ya Saa 4 asubuhi hadi Saa 8 mchana wanafunzi wataweza kushirikiana  kuangalia na kusimulia na kujadili tukio ili kulielewa vizuri na kuandika ripoti madarasani kwao.

Tukio jingine kubwa la kupatwa kwa jua kama hili halitatokea jingine kwa miaka 15 ijayo, kwa hiyo tunahitaji kutumia fursa hili kwa ukamilifu.

Ili kluangalia kupatwa huko, kila mmoja atahitaji kutumia kikinga macho kinachochuja mwanga wa jua kiitwacho kitazamia jua.  Nihatari sana kuangalia jua kwa macho ya moja kwa moja au hata kutumia vichujio vingine vya kiza vilivyotengenezwa kibinafsi.

Kitazamia jua maalum ni kifaa rahisi kilichotengenezwa kutokana na kichuja nguvu ya jua ambacho kinaondoa mionzi haribifu kwa asilimia 99.999. Miwani hiyo maalum ya jua inaweza kutengenezwa Tanzania kwa gharama isiyozidi 500/= kila moja, ikiwemo kuchapa fremu za kadbodi na kichuja nguvu ya jua (polymer filter) kinachoagizwa kutoka Marekani.

Aidha wataalam wanaonya wananchi kutumia tahadhari kwa kutoanaglia tukio hilo moja kwa moja kwa macho yao kwani ni hatari na wanapaswa kutumia miwani maalum ya jua iliyotengenezwa maksusi kwa kazi hizo

Magazeti

Magazeti
















ULIMISS HII YA JOH MAKINI KAZITAJA COLLABO ZAKE ZA INTERNATIONAL ITAZAME HII VIDEO HAPA CHINI…

Sababu zinazifanya samaki kupungua ziwaTanganyika

Sababu zinazifanya samaki kupungua ziwaTanganyika

Sababu ya samaki kupungua Ziwa Tanganyika

ImageGETTY IMAGESImageWatu waliongezeka eneo hilo miaka ya 1990 kutokana na ongezeko la wakimbizi

Utafiti mpya umebaini kupungua pakubwa kwa idadi ya samaki katika Ziwa Tanganyika, mojawapo ya maziwa muhimu zaidi kwa uvuvi duniani, kumetokana na ongezeko la joto duniani katika karne moja iliyopita.

Ziwa Tanganyika ndilo la kale zaidi Afrika na samaki wake huwa muhimu sana kwa lishe katika mataifa yanayopakana na ziwa hilo.

Lakini idadi ya samaki imepungua sana, huku wavuvi wakiendelea kuongezeka.

Ongezeko hili la wavuvi lilidhaniwa kuwa chanzo kikubwa cha kupungua kwa idadi ya samaki.

Lakini utafiti mpya unaonesha chanzo hasa ni ongezeko la joto duniani kutokana na mabadiliko ya tabia nchi.

Ziwa Tanyanyika ndilo la pili kwa ukubwa duniani miongoni mwa maziwa yenye maji yasiyo na chumvi na maji yake huwa katika mataifa manne: Burundi, Jamhuri ya KIdemokrasia ya Congo, Tanzania na Zambia.

Samaki kutoka kwa ziwa hilo hutoa asilimia 60 ya protini zitokanazo na wanyama ambazo huliwa na watu eneo hilo.

Aidha, ni eneo lenye aina nyingi ya wanyama na mimea.

ImageGETTY IMAGESImageSamaki kutoka Ziwa Tanganyika hutegemewa sana na wakazi

Ili kufahamu mabadiliko yanayotokea katika ziwa hilo, watafiti wamechukua sampuli za mchanga kutoka kwenye kina cha ziwa hilo.

Baada ya kufanya utathmini wa mchanga huo na visukuku, wamepata viashiria kwamba idadi ya samaki imekuwa ikishuka sambamba na ongezeko la joto duniani.

Wanasayansi wanasema katika maziwa yanayopatikana maeneo yenye joto karibu na ikweta, ongezeko la joto katika maji hupunguza kuchanganyikana kwa maji kutoka sehemu ya juu ya ziwa ambayo huwa na oksijeni pamoja na maji yenye virutubisho vingi sehemu ya chini kwenye ziwa.

Kutochanganyikana vyema kwa maji haya husababisha virutubisho vinavyofika juu kwenye ziwa kupungua, hili hupunguza ukuaji wa miani (mimea ya rangi ya kijani, kahawia au nyekundu inayoota chini ya bahari) na hili hupelekea kupungua kwa lishe ya samaki.

Watafiti waliohusika katika utafiti huo wanasema ongezeko la joto limepunguza kuchanganyikana kwa maji, kupungua kwa ukuaji wa miani pamoja na kupungua kwa maeneo ambayo viumbe waishio chini ya bahari wanaweza kuishi na kustawi.

"Wazo letu lilikuwa kuchunguza visukuku na kubaini kushuka kwa idadi ya samaki kulianza wakati gani," anasema Prof Andrew Cohen kutoka Chuo Kikuu cha Arizona.

"Iwapo hili lilifanyika kabla ya kuanza kwa uvuvi wa kiviwanda miaka ya 1950, basi ungekuwa na ushahidi mkubwa kwamba hili halitokani na ongezeko la uvuvi na hivi ndivyo tulivyobaini."

Wanasayansi hao hata hivyo hawajapuuzilia mbali athari za ongezeko la uvuvi katika miongo sita iliyopita.

Wanasema kumekuwa an ongezeko la watu tangu miaka ya 1990, hasa kutokana na wakimbizi waliotoroka mizozo na kuhamia maeneo yaliyo karibu na ziwa hilo.

ImageGETTY IMAGESImageWavuvi hutumia taa kuwavutia dagaa, ambao ndio sana huvuliwa kutoka kwenye ziwa hilo

"Ukizingatia mtindo wa sasa wa kuendelea kugawika zaidi kwa maji kwenye ziwa, idadi ya samaki itaendelea kupungua. Watu wanaosimamia sera wanafaa kuanza kufikiria kuhusu chanzo mbadala cha mapato na lishe kwa watu wanaoishi eneo hilo."

Matokeo ya utafiti huo yamechapishwa katika jarida la kisayansi la Proceedings of the National Academy of Sciences.

 Alikiba atakuwa msanii wa kwanza kutokea kwenye jarida maarufu la The Source la nchini Marekani.

Alikiba kutokea kwenye jarida la The Source la Marekani

The Source ni jarida maarufu kwa hip hop na limekuwa na heshima kubwa kwa muda mrefu. Kiba atakuwa mmoja wa wasanii wachache sana wa Afrika kuwahi kuandikwa kwenye jarida hilo.

Ameshare habari hiyo njema kwenye mtandao wa Instagram.

“The 1st Bongo Flava artist in history to be featured in the THE SOURCE MAGAZINE! I’m proud to place BongoFlava on cover feature of the number #1 MusicMag on the Planet,” aliandika msanii huyo wa Sony Music.

Hata hivyo hajasema makala yake itatokea kwenye toleo la mwezi gani.

The Source hutoka kila mwezi na kuandika zaidi habari za hip hop, utamaduni na siasa na lilianzishwa mwaka 1988. Ndio jarida la rap lililodumu kwa miaka mingi zaidi.


wema sepetu amtakia happy birth  Mtoto Tiffa wa Diamond

wema sepetu amtakia happy birth Mtoto Tiffa wa Diamond

August 6, 2016

Salam za Wema Sepetu kwa mtoto wa Diamond Platnumz 'Tiffa

August 6, 2016 ni siku ambayo anazaliwa mtoto wa staa wa kutokea  bongo fleva Diamond Platnumzambapo pamoja na watu wengi kumtakia kila la kheri  yupo pia mremboWema Sepetu ambaye kwenye akaunti yake ya Instagram amepost picha ya Mtoto wa  Diamond akayaandika haya>>>Happy Birthday Princess Tee…🎈🎉🎁🎊🎀💝 May Allah bless your precious lil self… You will definitely turn out to be a phenomenal young woman’– Wema Sepetu

Makonda awakabidhi rungu FFU kudhibiti UKUTA


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewapa rungu askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) mkoani hapa kuwadhibiti watakaothubutu kufanya maandamano ya kuunga mkono operesheni ya Chadema iliyopewa jina la Umoja wa Kupambana na Udikteta Tanzania (Ukuta).

Chadema walizindua operesheni hiyo na kutoa maazimio matatu ambayo yatatekelezwa  nchi nzima ikiwamo mikutano ya hadhara ambayo itafanyika Septemba Mosi, mwaka huu.

Wanadai wanataka kuzuia matukio ya ukandamizaji wa haki na demokrasia nchini inayofanywa na Rais, John Magufuli. Akizungumza jijini Dar es Salaam baada ya kukitembelea kikosi cha FFU Ukonga jana,  Makonda aliwataka askari wajipange kudhibiti Ukuta na hawana haja ya kusubiri maagizo kutoka kwa kiongozi yeyote.

Kategori

Kategori