WALAJI WA NYAMA YA NGURUWE HATARINI KUUGUA KIFAFA

Chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Kimehadhalisha walaji wa nyama ya Nguruwe nchini kuwa wanakabiliwa na hatari ya kupata kifafa. Utafiti wa kisayansi uliofanywa na SUA umebaini kuwa baadhi ya Nguruwe wana minyoo aina ya Tegu ambao nyama yao ikiliwa bila kuiva vizuri, mlaji atapata minyoo hiyo ambayo huingia kichwani na kusababisha kifafa.
Mhadhiri na Mtafiti Idara ya sayansi ya Wanyama na Uzalisha ya SUA, Profesa Faustine Lekule, alisema sampuli za utafiti huo kutoka Mbeya zimebaini Nguruwe wakiwamo wanaosafirishwa katika miji mikubwa wameathirika na minyoo hiyo.
Kwa mujibu wa Prof. Lekule, wataalamu wa SUA wanaosimamia mradi wa utafiti wa kuboresha ufugaji wa Nguruwe kwa mkoa wa Mbeya ili kuinua pato la kaya, unaofadhiliwa na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Denmark (DANIDA), walibaini hatari hiyo baada ya kuchukua sampuli ya nyama ya Nguruwe kwa ajili ya vipimo. "Majibu ya Sampuli ambazo wataalamu wamezichukua kutoka kwa Nguruwe wa wafugaji kwenye baadhi ya vijiji, wamebainika kukumbwa na hatari hii. Lazima jitihada za makusudi zichukuliwe katika kutafuta ufumbuzi wa pamoja wa tatizo hili kati ya watafiti na serikali" alisema Profesa Lekule.
Alisema maambukizi ya tegu au minyoo ya Nguruwe yanatokana na tabia za baadhi ya wafugaji kutozingatia ufugaji bora kwa kuwaacha Nguruwe kujitafutia chakula na maji mitaana na kula kinyesi cha binadamu.
Kwa mujibu wa Prof. Lekule, baadhi ya wafugaji wamekuwa wakijisaidia vichakani na kuwaacha Nguruwe kutafuta malisho ktk vichaka na kula kinyesi chao, hali inayochangia ongezeko la maambukizi ya minyoo ya tegu hao. Baada ya kula kinyesi minyoo humwingia mwilini na kumdhoofisha na baadaye binadamu anapokula nyama ambayo haijaiva vizuri minyoo hiyo humwingia na kusababisha kifafa baada ya kuingia kichwani.
Alisema athari za kuenea kwa maambukizi hayo inaweza kutokea ktk miji mikubwa ikiwamo Dar es salaam kwa kuwa nguruwe wa Mbeya husafirishwa na kuuzwa maeneo hayo. "Hatua hii inaweza kusababisha kusambaa kwa ugonjwa huu" alisema Profesa Lekule.
WALAJI WA NYAMA YA NGURUWE HATARINI KUUGUA KIFAFA .SUA yabaini hili soma zaid

WANAWAKE NAO WANATATIZO LA NGUVU ZA KIKE SOMA HAPA UJUE
Wanawake nao wana upungufu wa nguvu za kike
Safu hii inaendelea kuwaletea elimu kubwa ili kuwaweka wasomaji wake kwenye uelewa mkubwa kuhusu mapenzi na maisha.
INAVYOJULIKANA
Mara nyingi wanaume wamekuwa wakitajwa kama sababu kubwa ya wanawake kutofika katika matarajio ya safari ya tendo la ndoa pindi wanaposhiriki.
Hii inatokana na ukweli wa kibaiolojia kuwa, mwanaume wa kawaida hufika mwisho ndani ya wastani wa dakika 2.3 hadi 5 wakati mwanamke hufika kwa wastani wa dakika 15 hadi 20.
TABIA ZA WOTE
Ukiachilia mbali utofauti huo wa dakika, pia mwanaume wa kawaida mara baada ya kufikia mwisho hutumia dakika 15 hadi 30 ili aweze kurudia tena lakini kwa mwanamke huwa tofauti kwani huweza kuendelea zaidi bila kuwa na muda huo wa mapumziko.
Hivyo basi kwa tafsiri ya kawaida, mwanaume ana kawaida ya kuwahi kufika mwisho huku mwingine akiweza kurudia hadi pale mwanamke naye atakapofika.
Wanaume wenye matatizo yanayotajwa kama upungufu wa nguvu za kiume wakishindwa kurudia tendo hilo hubeba lawama za kutowaridhisha wapenzi wao au wake zao.
UTAFITI WA KARIBUNI
Hata hivyo, tafiti mbalimbali za hivi karibuni zimebaini kuwa, asilimia 31 tu ya wanaume ndiyo wana matatizo ya upungufu wa nguvu za kiume huku wanawake wao, asilimia 43 wakitajwa kuwa na matatizo yanayowasababishia kutofika mwisho kitaalamu female sexual dysfunction ‘FSD’ ambayo hata mwanaume awe rijali kiasi gani hushindwa kumfikisha mwisho mwanamke mwenye matatizo hayo.
Mbaya zaidi, wanawake wengi hawana ufahamu wa tatizo hilo kwa kuwa hakuna elimu ya kutosha kwenye jamii, suala linalowafanya watoe lawama kwa wapenzi wao jambo ambalo si sahihi bali wana upungufu wa nguvu zao wenyewe.
SABABU ZA TATIZO
FSD kwa wanawake husababishwa na matatizo mbalimbali kama vile magonjwa ya kisukari, moyo, matatizo ya mishipa ya fahamu, matatizo ya homoni, mapafu, ini, utumiaji wa madawa ya kulevya, utumiaji wa baadhi ya madawa makali bila ushauri wa daktari, ajali na sababu nyinginezo kama vile matatizo ya kisaikolojia.
ATHARI ZAKE
Matokeo ya mwanamke kuwa na ugonjwa huu ni kutokuwa na hamu ya kufanya mapenzi hata kama yupo ndani ya ndoa, kuchukua muda mrefu kupata hisia hizo au kutopata kabisa, kuchelewa kuliko kawaida kufika mwisho au kutofika kabisa.
Pia kuchoka, kutosikia ladha ya mapenzi au kuwa na maumivu wakati wa tendo la ndoa.
Hivyo basi ni vyema kama mwanamke atakuwa na dalili hizo afike katika vituo vya afya kwa ajili ya matibabu ya kitaalam.
socre:dullonet.com
Source;Chizika